Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamlaka za Nigeria zimeripotiwa kuwazuilia maafisa wakuu wa Binance

Mamlaka Za Nigeria Zimeripotiwa Kuwazuilia Maafisa Wakuu Wa Binance Mamlaka za Nigeria zimeripotiwa kuwazuilia maafisa wakuu wa Binance

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Mamlaka ya Nigeria hapo jana iliripotiwa kuwaweka kizuizini watendaji kutoka jukwaa la kimataifa la kubadilishana sarafu ya crypto Binance kwa madai ya "kurekebisha kiwango cha ubadilishaji wa nchi".

Taarifa za kukamatwa kwa watendaji hao wawili bado ni tete.

Hata hivyo, ripoti zinasema walikuwa wamefika Nigeria kujadili kusimamishwa kwa jukwaa la biashara na mamlaka ya Nigeria.

Gavana wa Benki Kuu ya nchi hiyo, Olayemi Cardoso, Jumanne alifichua kwamba takriban $26bn (£20bn) zilipitia Binance Nigeria katika biashara ya sarafu ya fiche kupitia "vyanzo na watumiaji ambao hatuwezi kuwatambua vya kutosha".

Katika mahojiano ya Jumatano kwenye Kituo cha Televisheni cha ndani, Bayo Onanuga, msemaji wa rais, alishutumu jukwaa la crypto kwa kurekebisha viwango vya ubadilishaji wa nchi na kuchukua jukumu la benki kuu.

"Ikiwa hatutamshikilia Binance, Binance ataharibu uchumi wa nchi hii. Wanarekebisha kiwango tu,” aliongeza. Maafisa wa Binance bado hawajajibu madai hayo.

Desemba mwaka jana, mamlaka ya Nigeria iliondoa marufuku ya miaka miwili iliyowekwa kwa miamala ya sarafu-fiche kutokana na kile walichokitaja kuwa hatari za utakatishaji fedha na ufadhili wa ugaidi unaotokana na sarafu ya fiche nchini humo.

Hatua hii ya serikali dhidi ya Binance ni miongoni mwa hatua inazoamini zingeokoa sarafu ya ndani ya naira, ambayo imeshuka thamani kwa karibu 70% katika miezi minane iliyopita.

Chanzo: Bbc