Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamlaka Kenya zachunguza ugonjwa usiojulikana uliowakumba watoto 95

Rais Ruto Apata Pigo, Aambiwa Nyadhfa 50 Za Mawaziri Si Halali Mamlaka Kenya zachunguza ugonjwa usiojulikana uliowakumba watoto 95

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: Voa

Mamlaka ya afya nchini Kenya inachunguza ugonjwa usiojulikana baada ya zaidi ya wanafunzi 90 wa shule za upili kulazwa katika hospitali mbalimbali za Kakamega, Magharibi mwa Kenya.

Wanafunzi hao kutoka Shule ya Upili ya Wasichana ya Eregi walikuwa na dalili za maumivu ya goti na walikuwa na ugumu wa kutembea.

Jared Obiero, afisa mkuu wa elimu, aliwahakikishia wazazi waliofika shuleni kwamba hali imedhibitiwa.

"Sote tumekubaliana kwamba hatuwapeleki watoto wetu nyumbani, watasimamiwa kutoka hapa. Idara ya elimu, serikali ya kaunti na idara ya afya ya umma wanatoa ahadi kwamba watoto hao watatibiwa,” akasema.

Sampuli za damu, mkojo na kinyesi zilitumwa kwa maabara katika jiji jirani la Kisumu na mji mkuu, Nairobi.

Matokeo ya mwisho ya kuamua sababu ya ugonjwa huo yanatarajiwa, Jumatano, Oktoba 4.

Chanzo: Voa