Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamlaka Kenya yakana taarifa kuwa askari wake wameuawa Haiti

Mamlaka Kenya Yakana Taarifa Kuwa Askari Wake Wameuawa Haiti.png Mamlaka Kenya yakana taarifa kuwa askari wake wameuawa Haiti

Mon, 1 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa huduma za polisi nchini Kenya amekana taarifa alizoziita za uongo, zisizo za kizalendo na zisizo za msingi zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa, askari wake wameuawa nchini Haiti.

''Tunapenda kuufafanulia Umma kuwa maafisa wetu waliondoka Kenya tarehe 24 mwezi Juni mwaka 2024 na si tu kuwa walikaribishwa kwa ukarimu na watu wa Haiti, lakini pia wako na tayari wako kwa ajili ya kutekeleza jukumu lao, Ilisema sehemu ya taarifa.

''Tunapenda kurejelea tena kuwa misheni yetu nchini Haiti ni kwa ajili ya raia wa Haiti, na tunapenda kuomba wakenya wenzetu kuwaunga mkono kwa kupeperusha juu bendera ya nchi yetu, sambamba na kutekeleza majukumu yao kimataifa. Ilisema taarifa hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live