Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamilioni ya fedha zilizoibwa na kufichwa visiwani kurejeshwa nchini

Wash Wash Kenya KRA Mamilioni ya fedha zilizoibwa na kufichwa visiwani kurejeshwa nchini

Tue, 29 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamilioni ya pesa za umma zinazodaiwa kuibwa na matajiri wawili wa Kenya zinatarajiwa kurejeshwa nchini humo kununua vifaa vya kjupambana na Covid-19 kufuatia kesi ya kihistoria.

Makubaliano hayo yaliyofanyika Jersey, kisiwa kinacho jitawala Uingereza, yametajwa kuwa ni "ushindi kwa watu wa Kenya" na balozi wao wa Kenya nchini Uingereza, Manoah Esipisu.

Mtandao huu wa utapeli uliibuka mara kwanza katika kesi ya talaka ya mwaka 2006, baada ya Samuel Gichuru, bosi tajiri wa kampuni ya umeme ya Kenya, na mkewe Salome Njeri walipo talikiana.

Ilipofikia wakati wa kugawanya mali zao, Bi Njeri alihisi kuwa hapati mgawo wake sawa.

Alidai baadhi ya mali za mumewe zilikuwa zimefichwa ili zisisikilizwe na, kortini, aliorodhesha maelezo ya akaunti alizodai kuwa ni za Bw Gichuru huko Jersey, ambayo mara nyingi huhusishwa na akaunti za siri za nje ya nchi na mazingira ya ushuru mdogo.

Hilo lilizua uchunguzi wa miaka tisa na mamlaka ya Jersey katika maeneo 12 ya mamlaka.

Kama sehemu ya uchunguzi huo, mwaka wa 2011, walimshutumu Bw Gichuru na aliyekuwa Waziri wa Fedha Chris Okemo kwa kuchukua pesa kutoka kwa mashirika ya kimataifa ambayo yalitumwa kwa kampuni iliyosajiliwa Jersey.

Mamlaka ya Jersey ilitoa vibali vya kukamatwa kwa wanaume wote wawili na wamekuwa wakisubiri kurejeshwa Kenya tangu wakati huo.

Uhalifu wa kiuchumi waliotuhumiwa nao ni pamoja na makubaliano na kampuni ya Kifini ya kujenga kituo cha umeme karibu na Mombasa, jiji la pili kwa ukubwa nchini Kenya, na kuchukua mamilioni ya pauni kama rushwa kutoka kwa makampuni ya uhandisi ya Uingereza, Norway na Ujerumani, pamoja na kampuni kubwa ya mawasiliano ya Marekani. .

Licha ya BBC kujaribu mara kwa marakuwasiliana nao, matajiri hao na mawakili wao hawakutoa maoni yoyote kuhusu tuhuma zinazotolewa dhidi yao.

Hata hivyo mwaka 2016, kampuni iliyosajiliwa huko Jersey ya Windward Trading Limited ilikubali mashtaka manne ya utakatishaji fedha haramu katika mahakama ya Jersey.

Mahakama iliamua kwamba kampuni hiyo, ambayo mmiliki wake mkuu alikuwa Bw Gichuru, inapaswa kunyang'anywa zaidi ya dola milioni 4.9m (£3.6m) za mali kwa utakatishaji wa pesa.

Pesa hizo nyingi ndizo zinazodaiwa kutokana na ufisadi nchini Kenya kati ya mwaka 1999 na 2002 ambazo sasa zinarejeshwa nchini.

Hilo liliwezeshwa katika makubaliano ya 2018 yaliyotiwa saini nchini Kenya na Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo Theresa May, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na serikali za Uswizi na Jersey.

Katika mpango huo, ilibainika kuwa mali zinazodaiwa kuibiwa zinaweza kurejeshwa nchini Kenya, mradi tu zitumike kwa miradi ya maendeleo pekee.

Mpango huu, unaojulikana kama Mfumo wa Kurudisha Mali zilizotokana na Ufisadi na Uhalifu hadi Kenya (Fracck), ulisifiwa na Umoja wa Mataifa kwa"ubunifu"

Inaipa Jersey mamlaka ya kutoa leseni ya kufungia pesa ambazo wanaamini ziliibwa na kuzirudisha kabla ya wale wanaoshutumiwa kuziiba kusomewa mashtaka.

"Swali kwetu [kwaJersey] lilikuwa: je, tungojee mchakato wa kimahakama uliovurugika kulingana na vitendo vya watu wawili, ambao... wameonekana kuwa kinyume cha sheria katika mahakama ya Jersey? Au turuhusu pesa zirudishwe kwa ajili ya manufaa ya raia wa Kenya?" Seneta Ian Gorst, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jersey, alieleza.

Kukabidhiwa kwa mamilioni ya pesa za Bw Gichuru zinazodaiwa kuibwa na kuwarudishia Wakenya wa kawaida ni mtihani wa kwanza wa Fracck.

Kuitumia kwa uwazi na uwajibikaji ni kazi kampuni ya Crown Agents, Kampuni ya isiyo ya kibiashara ya maendeleo ya kimataifa

Bosi wake Fergus Drake aliambia BBC kwamba alikuwa akiwasiliana na wizara ya afya ya Kenya ili kutathmini kile kinachohitajika katika vita dhidi ya Covid-19.

Alisema ilitaka "vifaa maalum vya maabara kupima Covid-19" na vifaa vya ziada "kama mirija ndogo, vipimo vya PCR, na vifaa vingine".

Bw Drake anatarajia kupeleka vifaa hivyo muhimu kwa nusu dazeni ya hospitali katika muda wa miezi miwili.

Alisema kuongeza upimaji kutaruhusu Wakenya kudhibiti vyema janga hili na kujua ni maeneo gani yanahitaji chanjo ya haraka.

Kwa sasa, chini ya asilimia 20 ya Wakenya wamechanjwa kikamilifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live