Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamilioni ya Wanigeria waandamana

Ya Wanigeria Mamilioni ya Wanigeria waandamana

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamilioni ya Wanigeria hawana umeme baada ya gridi ya taifa kuzimwa kama sehemu ya mgomo wa taifa kuhusu kupanda kwa gharama ya maisha.

Nchi ilitumbukia gizani kwa muda usio pungua Saa 24 wakati wanachama wa vyama vya wafanyakazi walipozuia wahudumu katika vyumba vya kudhibiti umeme nchini humo kufanya kazi na kuzima vituo vidogo vya umeme.

Safari nyingi za ndege zimesitishwa katika uwanja wa ndege wenye shughuli nyingi zaidi nchini humo mjini Lagos, na katika mji mkuu, Abuja huku abiria wakiwa wamekwama.

Vyama vya wafanyakazi vinadai nyongeza kubwa ya kima cha chini cha mshahara, vikisema wafanyakazi hawawezi kuishi kwa kiwango cha sasa cha naira 30,000 sawa na dola 22 za kimarekani sawa na Tsh 61,000 kwa mwezi.

Pia wametoa wito kwa serikali iwafikirie na kuongeza kima cha chini cha mshahara ili waweze kuishi na kula chakula kizuri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live