Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamia ya wapiganaji wa ADF wameuawa katika mashambulizi Uganda - Museveni

Mamia Ya Wapiganaji Wa ADF Wameuawa Katika Mashambulizi Uganda   Museveni Mamia ya wapiganaji wa ADF wameuawa katika mashambulizi Uganda - Museveni

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Wanajeshi wa Uganda waliwauwa wapiganaji 200 wa ADF katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wakati operesheni za kijeshi za kuwaondoa wanamgambo wa kundi la Islamic State zikiendelea, rais wa Uganda alisema.

"Tumekuwa tukifanya mashambulizi ya anga dhidi ya magaidi nchini Congo," Rais Yoweri Museveni alisema kwenye mtandao wa X, zamani wa Twitter, akiongeza kuwa karibu "200 kati yao waliuawa" katika mashambulizi yaliyofanywa tarehe 16 Septemba.

Mashambulizi zaidi dhidi ya wapiganaji hao yametekelezwa tangu wakati huo, Bw Museveni aliongeza, bila kutoa maelezo zaidi.

Msemaji wa jeshi la Uganda Felix Kulayigye ameliambia shirika la habari la AFP kwamba rais alikuwa akimaanisha wapiganaji wa kijihadi wa kundi la ADF.

Mnamo mwaka wa 2021, Uganda na DR Congo zilianzisha mashambulizi ya pamoja ya kijeshi dhidi ya ADF mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, lakini kundi hilo bado linafanya mashambulizi katika nchi zote mbili.

Mnamo Oktoba, watalii wawili, mwanamume wa Uingereza na mwanamke wa Afrika Kusini kwenye fungate yao, pamoja na kiongozi wao, waliuawa walipokuwa safarini katika Mbuga ya Kitaifa ya Malkia Elizabeth nchini Uganda.

Kundi la Islamic State lilidai kuhusika na shambulio hilo. Mwezi Juni, watu 42, wakiwemo wanafunzi 37, waliuawa katika shambulio dhidi ya shule ya sekondari magharibi mwa Uganda, ambalo pia lilihusishwa na ADF.

Chanzo: Bbc