Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamia ya wanamgambo wa Jihadi wafanya mashambulizi Niger

Mamia Ya Wanamgambo Wa Jihadi Wafanya Mashambulizi Niger Mamia ya wanamgambo wa Jihadi wafanya mashambulizi Niger

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Serikali nchini Niger imesema takriban wanajeshi 12 wamefariki baada ya kushambuliwa na watu wanaoshukiwa kuwa wananmgambo wa jihadi kusini-magharibi mwa nchi hiyo.

Wizara ya ulinzi imesema wanajeshi saba waliuawa katika mapigano, wakati kikosi chao kiliposhambuliwa na mamia ya waasi waliokuwa kwenye pikipiki katika mji wa Kandadji.

Wengine watano walifariki katika ajali ya barabarani walipokuwa wakijaribu kuja kusaidia kitengo hicho.

Washirika wa ndani wa al-Qaeda na kundi la Islamic State wanafanya kazi katika eneo hilo - ambalo liko karibu na mpaka wa Mali na Burkina Faso

Chanzo: Bbc