Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamia ya Wahamiaji waliuawa na walinzi wa mpaka wa Saudi Arabia– ripoti

D2f86c4d 9332 4043 A8a6 8eb3797a0bb7 Mamia ya Wahamiaji waliuawa na walinzi wa mpaka wa Saudi Arabia– ripoti

Mon, 21 Aug 2023 Chanzo: Voa

Walinzi wa mpaka wa Saudi wanatuhumiwa kwa mauaji ya umati ya wahamiaji kwenye mpaka wa Yemen katika ripoti mpya ya Human Rights Watch.

Ripoti hiyo inasema mamia ya watu, wengi wao wakiwa ni Waethiopia wanaovuka Yemen inayokumbwa na vita ili kufika Saudi Arabia, wameuawa kwa kupigwa risasi.

Wahamiaji wameiambia BBC kwamba walikatwa miguu na mikono kwa risasi na waliona miili iliyoachwa kwenye njia.

Awali Saudi Arabia ilikana madai ya mauaji yaliyopangwa.

Ripoti ya Human Rights Watch (HRW) iliyopewa jina la They Fired On Us Us Like Rain, ina ushuhuda wa wazi kutoka kwa wahamiaji ambao wanasema walipigwa risasi na wakati mwingine kulengwa kwa mashambulizi ya milipuko kutoka kwa polisi na wanajeshi wa Saudia kwenye mpaka wa kaskazini mwa Yemen na Saudi Arabia.

Wahamiaji waliowasiliana kando na BBC wamezungumza kuhusu vivuko vya kutisha wakati wa usiku ambapo makundi makubwa ya Waethiopia, wakiwemo wanawake wengi na watoto, walishambuliwa walipojaribu kuvuka mpaka kutafuta kazi katika ufalme huo wenye utajiri wa mafuta.

"Milio ya risasi iliendelea na kuendelea," Mustafa Soufia Mohammed mwenye umri wa miaka 21 aliiambia BBC.

Alisema baadhi katika kikundi lake la wahamiaji 45 waliuawa waliposhambuliwa na risasi walipokuwa wakijaribu kuvuka mpaka Julai mwaka jana.

Chanzo: Voa