Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamia waripotiwa kufariki wakati wa mgomo katika hospitali huko Msumbiji

Mamia Waripotiwa Kufariki Wakati Wa Mgomo Katika Hospitali Huko Msumbiji Mamia waripotiwa kufariki wakati wa mgomo katika hospitali huko Msumbiji

Mon, 21 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Takribani watu 620 wanaripotiwa kufariki katika Hospitali Kuu ya Maputo katika siku 40 zilizopita kutokana na mgomo wa wahudumu wa afya.

Madaktari wa Msumbiji wamegoma kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo, na madaktari haswa wameongeza mgomo wao kwa siku 21 zaidi licha ya kutishiwa kuuawa.

Wakati huu huduma ya chini itatolewa kwa wagonjwa, madaktari wanasema, "ili watu wetu wasiteseke tena". Wafanyakazi wanaogoma wanasema wanakosa dawa na vifaa muhimu na hata wanapaswa kulipa kutoka mifukoni mwao kununua ambulensi zenye vifaa vya kimsingi.

Wanasema hawana budi ila kugoma na wanataka Waziri wa Afya Armindo Tiago atimuliwe kazi, hata hivyo, inasema inasikitika kwamba madaktari wamechukua uamuzi wa kurefusha mgomo wao licha ya maendeleo ambayo inasema wamefanya katika kutimiza matakwa yao.

Chanzo: Bbc