Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamia waandamana wakitaka Rais wa zamani wa Afrika Kusini kuachiliwa huru

6ab14465339950a5 Mamia waandamana wakitaka Rais wa zamani wa Afrika Kusini kuachiliwa huru

Wed, 14 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Watu 45 wamefariki dunia kwenye ghasia zinazoendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini Afrika Kusini kufuatia kukamatwa kwa rais wa zamani wa nchi hiyo, Jacob Zuma.

Habari Nyingie: Polisi Achanganyikiwa Baada ya Wezi wa Kutumia Bodaboda Kumpokonya Simu Wakati Akizungumza

Kufikia sasa watu 800 wamekamatwa kwa madai kwamba wamekuwa wakiendesha maandamano nchini humo.

Waandamanaji walichoma magurundumu, wakafunga barabara kuu za miji ya nchi hiyo, wakavamia wananchi na kupora maduka.

Serikali ya Afrika Kusini imelipelekwa jeshi katika maeneo mbalimbali kuongeza nguvu na kusaidiana na polisi kuzima ghasia hizo.

Waziri wa Polisi Bheki Cele amewaambia waandishi wa habari kwamba uporaji unaendelea na ipo hofu kwamba, kuna baadhi ya maeneo yatakuwa na uhaba wa bidhaa za msingi.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.



Read also

COVID-19: Watu 761 Zaidi Wakutwa na Virusi Huku 9 Wakiangamia
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke