Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo matatu kuhusu Hayati Magufuli

E0d0217105f0326f2b30d690081bc4a0 Mambo matatu kuhusu Hayati Magufuli

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema Hayati Rais John Magufuli atakumbukwa kwa mambo matatu muhimu ikiwemo kuwa shujaa katika mapambano dhidi ya ufisadi na rushwa.

Ameyasema hayo mjini Dodoma wakati akitoa salamu zake za kufuatia kifo cha Rais Magufuli kilichotokea Machi 17 mwaka huu kwenye Hospitali ya Mzena Dar es Salaam kwa tatizo la mfumo wa umeme wa moyo.

Ramaphosa alitaja mambo ambayo Magufuli atakumbukwa nayo ni alikuwa moja ya kizazi kipya cha uongozi katika Bara la Afrika ambaye si tu kwamba alianzisha vita dhidi ya ufisadi na rushwa, bali pia aliamini kuwa viongozi wanapaswa kufanya kazi kwa ajili ya watu wao na si kwa ajili yao wenyewe.

“Pia namshukuru kwa juhudi zake za kuelekea ukombozi na mafanikio ya kiuchumi kwa nchi yake, kikanda na bara zima, alikuwa Kiongozi aliyetaka masuala ya tamaduni, mila na desturi yatumike kutatua changamoto mbalimbali zilizopo,”alisema Rais Ramaphosa.

Alisema Rais Magufuli hakupenda kusafiri sana na badala yake alipenda kubaki hapa nchini ili aendelee kuwatumikia Watanzania.

“Nilijisikia kuheshimiwa sana kwa sababu Rais Magufuli hakuwa msafiri mkubwa, hakupenda kusafiri sana, alipendelea sana kubaki hapa nyumbani, nilidhani labda alikuwa anaogopa kusafiri kwa ndege, lakini aliniambia hapana, bali alipendelea kubaki nchini ili aendelee kuwatumikia wananchi wa Tanzania badala kusafiri kila upande,”alisema Ramaphosa na kuongeza

“Rais Magufuli aliamua kubaki hapa nyumbani kuwatumikia ninyi Watanzania na mambo aliyoyafanya yanavutia na hakika mlikuwa Taifa lenye bahati kuwa na kiongozi kama John Magufuli.”

Chanzo: www.habarileo.co.tz