Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo Saba Usiyoyajua Kuhusu Rais Mugabe

Mugabe 1?fit=800%2C544&ssl=1 Mambo Saba Usiyoyajua Kuhusu Rais Mugabe

Thu, 13 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msomaji wetu natumaini ni mzima wa afya na leo katika listi tumekusogezea mambo saba usiyoyajua kuhusu marehemu Robert Mugabe ambaye aliwahi kuwa Rais wa Zimbabwe.

Mugabe alifariki dunia Septemba 6, 2019 akiwa na umri wa miaka 95 na umauti ulimfika nchini Singapore akipokea matibabu kwa muda mrefu.

Mwanasiasa huyu machachari aliiongoza Zimbabwe kutoka 1980 mpaka 2017, alipong'olewa madarakani na makamo wake kwa msaada wa jeshi.

Mugabe alizaliwa katika kijiji cha Kutama, Kusini-Magharibi mwa jiji kuu Harare, alisomeshwa na wayesuti, na baadaye akawa mwalimu kabla kujiingiza katika harakati za kupigania uhuru wa Zimbabwe.

Uwanaharakati wake ulimfanya afungwe gerezani kwa miaka 11, na baadaye mwaka 1980 akawa rais wa kwanza wa Zimbabwe.

Yafuatayo ni mambo saba ambayo huenda hukuwa wayajua kumhusu kiongozi huyu-na ambayo huenda yalimuwezesha kuwa rais kwa muda mrefu mno.

1. Alikuwa mpenda mazoezi na vyakula vya kienyeji

Unaambiwa kuwa Mugabe alikuwa anapenda kufanya mazoezi. “Mimi hujihisi mgonjwa wakati sijafanya mazoezi ya viuongo vya mwili,” Mugabe aliwahi kusema hayo

Huwa anaamuka kati ya saa kumi na kumi na moja alfajiri, na kutokana na jamaa zake wa karibu, husikiliza BBC idhaa ya dunia.

Siri nyingine ya kuishi kwake kwa muda mrefu ni kuwa alikuwa akipenda sana-chakula cha kienyeji kinacholiwa sana Zimbabwe. Kisha pia, havuti sigara, ila hunywa pombe kidogo anapokula.

2. Alipata mtoto akiwa miaka 73 Mugabe alikuwa na watoto watatu na mke wake wa pili, Grace Marufu, aliyekuwa karani wake. Mtoto wao wa tatu alizaliwa 1997, mwaka mmoja baada ya wao kufunga ndoa.

Mwanawe wa kwanza, Nhamodzenyika, alikufa kutokana na Malaria akiwa miaka mitatu bado wakiwa Ghana. Mugabe alinyimwa ruhusa ya kuenda Accra kuungana na mkewe kwa mazishi ya mwanawe, kwani alikuwa mfungwa wa kisiasa wa serikali ya enzi hiyo ya Rhodesia.

3. 'Kufufuka' Ingawa kulikuwa na uvumi mara nyingi kuwa Mugabe hana afya nzuri, afya yake na kazi zake za kisiasa ziliendelea vyema kabisa.

Kuhusu afya yake Mugabe alipohojiwa wakati mmoja alisema,“ Nimekufa mara nyingi-hapo ndipo humwelekea Yesu Kristo. Yesu alikufa mara moja, na akafufuka mara moja,” alisema alipotimia miaka 88.

Ingawa alilelewa katika familia ya kikatoliki-mamake alikuwa mcha Mungu-alisema alipohojiwa na kituo cha habari cha Afrika Kusini, SABC, miaka michache iliyopita, kuwa yeye si Mkristo anayetumikia dini kwa sana.

4. Alikuwa Shabiki mkubwa sana wa kriketi Enzi za uhai wake Mugabe alidhihirisha hadharani mapenzi ya mchezo wa kriketi. Alikuwa ni patroni wa jumuiya ya mchezo wa kriketi wa Zimbabwe, ambapo nyumba yake ipo karibu na uga wa michezo wa Harare, na alikuwa anaweza kutazama kwa makini wakati wa michezo wa kitaifa.

“Kriketi yafanya watu wawe wangwana, na pia inawafanya watu kuwa wema,” Mugabe alisema miaka kadhaa baada ya Zimbabwe kujinyakulia uhuru. “Nataka kila mtu acheze kriketi Zimbabwe; nataka nchi ya Zimbabwe iwe nchi ya wangwana.”

5. Alikuwa hapendi kushindwa Unaambiwa alipokuwa kijana, Mugabe alikuwa mmakinifu na mzuri kabisa katika mchezo wa tennis,” alisema aliyekuwa mwalimu katika shule ya Wakatoliki alikosomea Mugabe. Ila, aliposhindwa katika mchezo huo, aliitupa raketi yake chini kwa hasira.

Mugabe alikiri kuwa hakuwa mzuri katika mchezo wa kandanda alipokuwa mdogo, ila enzi za uhai wake alipenda kuutazama mchezo huo.

Yeye alikuwa shabiki wa vilabu vya Chelsea na Barcelona vilivyoko Uingereza na Uhispania mtawalia. “Ninapotazama kandanda, sitaki usumbufu kutoka kwa mtu yeyote,” alisema mwaka 2012. “Hata mke wangu anajua mahala pa kukaa wakati wanapofunga bao uwanjani, hata mimi pia hufunga bao kwangu kwa kupiga mateke vitu vyovyote vilivyoko mbele yangu.”

6. Alikuwa ni mtu mwenye shahada nyingi Kwa jumla, Mugabe alikuwa na shahada saba. Digrii yake ya kwanza ni kutoka katika Chuo Kikuu cha Fort Hare kilichoko Afrika Kusini. Alisomea digrii zake zingine kwa njia Internet-mbili akiwa gerezani-shahada hizo ni za elimu, sayansi, sheria na usimamizi.

Amejitapa kuwa na “shahada katika ujuhula” alipokuwa akivionya vyama vya kutetea haki za wafanyakazi nchini Zimbabwe 1998 kila vilipotishia kugoma.

7. Alikuwa Mvaaji wa nguo maridadi Mugabe alikuwa anapenda sana suti zinazoutosha mwili wake kisawasawa na tai zinazofanana na kitambaa. Alikuwa akiwavutia sana wanamitindo nchini Zimbabwe kwa mavazi yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live