Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo Matano usiyoyajua ya kusisimua kuhusu Congo

Gettyimages 1244417934 2c955b87690fe3939dde9bfa6b9f3d6518e6718b Mambo Matano usiyoyajua ya kusisimua kuhusu Congo

Tue, 21 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

1. Asilimia 80 ya ardhi ya Congo inafaa kwa kilimo, ni nchi yenye eneo kubwa sawa na Ulaya Magharibi. (England, France, Germany, Italy, Netherland, Spain, Portugal, Belgium, Austria, nk.)

2. Congo ina hazina ya asilimia 10 ya shaba ya dunia nzima. Asilimia 30 ya cobalt ya dunia nzima, dhahabu, Almasi, Platinum, Bauxite, Lead (risasi), madini ya fedha, Zink, na inazalisha asilimia 80 ya madini ya Coltan yanayotumika kutengenezwa Simu, Sumaku, iPods, na injini za 'Jet'.

3. Congo pia ni tajiri kwa Uranium. Wakati wa vita kuu ya pili ya dunia, Marekani waliipiga miji miwili ya Japan kwa mabomu ya atomic, Hiroshima na Nagasaki. Mabomu yale yalitengenezwa kwa madini ya Uranium iliyoibwa Congo.

4. Mto Congo ni mto wa pili kwa Ukubwa duniani, una maporomoko (Inga water falls) yanayoweza kuzalisha umeme na kusambazwa Africa na Ulaya kwa Pamoja.

5. Kuna aina 1100 za madini katika nchi yote ya Congo, Utajiri wa madini peke yake unakaribia dola trilioni 24, sawa na uchumi wa marekani na Ulaya kwa Pamoja.

Hayo ni baadhi ya mambo ya kusisimua kuhusu Congo ambayo leo wananchi wake wanapitia mateso licha ya kuwa na utajiri mkubwa.

Wazungu wanasema "DR Congo: Cursed by its natural wealth" wakimaanisha "DR Congo: Imelaaniwa na utajiri wake wa asili"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live