Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama na bintiye wakamatwa Nairobi na bunduki hatari aina ya Uzi

Aa0380eeaf5e7f60 Mama na bintiye wakamatwa Nairobi na bunduki hatari aina ya Uzi

Thu, 15 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Makachero jijini Nairobi wamewatia mbaroni mama na bintiye ambao wanashukiwa kuhusika na shughuli za kigaidi humu nchini.

Wawili hao walikamatwa eneo la Racecourse jijini Nairobi na silaha ambazo makachero wametaja kama hatari sana.

Kulingana na ripoti ya DCI, wawili hao walikamatwa Jumatano Aprili 14 na kupatwa na bunduki aina ya Uzi Automatic Submachine ambayo ni hatari sana.

Aidha bastola na risasi kadhaa pia zilipatikana wakati wa oparesheni hiyo kali iliyofanywa chini na umakini mkubwa.

Wawili hao wametambuliwa kama Goretti Mwihia ba bintiye Joyce Muthoni Mwihia ambao wanaendelea kuhojiwa kuhusiana na silaha hizo.

Duru za polisi zimearifu kuwa kikosi cha maafisa wa kupambana na ugaidi humu nchini kimeitwa kuendeleza uchunguzi kuhsuu wawili hao.

Washukiwa hao wanaaminika wamekuwa wakisafiri nje na ndani ya taifa kwani wanamiliki uraia wa nchi nyingine.

Polisi wanasema inashukiwa silaha hizo zilikuwa zitumike katika kutekeleza mavamizi ya kigaidi humu nchini.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke