Mama mmoja nchini Uganda amezua gumzo la siku baada ya kusimulia ana watoto 44 na hajachoka kuwapata wengine.
Mama huyu mwenye jina Mariam Nabatanzi na mwenye umri wa mika 41 alisema watoto hao wote anawalea peke yake jambo lililowafanya wanajamii anakoishi kumpachika jina Mama Afrika au Mama Uganda.
Nabatanzi alisema watoto wake wote ni zao la uhusiano wake na mwanaume mmoja, ambaye alimtelekeza baada ya kuzaa watoto hao.
Alijifungua mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 13 tu baada ya kuozwa kwa wazazi wake kwa mwanamume mwenye umri wa miaka 57.
"Nilijifungua mara 15. Nilijifungua watoto wanne mara tano. Kwa mapacha ni mara sita, lakini pateni hiyo iliisha," mama huyo alisema.