Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama kambo wa Rais wa Zamani Barrack Obama, Keziah Aoko aaga dunia

5e98f456e9770a87 Mama kambo wa Rais wa Zamani Barrack Obama, Keziah Aoko aaga dunia

Wed, 14 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wiki chache baada ya kumpoteza bibi yake, Rais wa zamani wa Marekani Barrack Obama ameondokewa na mama wake wa kambo Keziah Aoko Obama.

Marehemu alikuwa mama wa kaka maarufu wa Barack Obama, Malik Abong’o Obama.

Aoko aliaga dunia Jumanne, Aprili 13, akipokea matibabu katika hospitali moja nchini Uingereza, familia yake imethibitisha.

Familia hiyo ikiongozwa na ndugu wengine wa Malik, Said Obama, ilisema marehemu mwenye miaka 81, amekuwa akiugua kwa muda kwa mujibu wa ripoti ya The Standard.

Msemaji wa marehemu Mama Sarah Obama, Nelson Ochieng, alimtaja Aoko kama mja ambaye alikuwa akibadilisha maisha ya wanaomzingita .

“Aliwagusa wengi katika kijiji cha Kogello. Alikuwa akituambia kila mara yeyote anaweza kuafikia ndoto yake," alisema Ochieng.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke