Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama awatoroka wanaye baada ya mumewe kufariki

Mk Jka Mama awatoroka wanaye baada ya mumewe kufariki

Mon, 9 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wasichana wawili wachanga waliachwa bila makao baada ya mama yao kuwakimbia punde kufuatia kifo cha baba yao.

Baba yao ambaye alikuwa ndiye wakutegemewa na familia hiyo alifariki dunia hospitalini baada ya kupata majeraha kufuatia ajali katika eneo lake la kazi.

Siku chache baada ya kumzika baba yao, madada hao kutoka Kavumu Avenue, Kiziba One katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, walisema mama yao aliondoka na hawajui aliko.

"Mama yetu alipanga virago vyake na kwenda kana kwamba anaenda kazini, lakini hakurudi tena. Hata hakutuaga ili kujua kwamba hatarudi. Tuliendelea kumsubiri tu arudi bila mafanikio.

"Siku zilipita wiki na miezi na ndipo tulipogundua kwamba alituacha kabisa, na ukutokuwa na uwezekano wa kurudi," Natalie, mmoja wa watoto hao aliambia Afrimax English.

Natalie na dada yake hawaendi shule, hawana chanzo cha mapato au jamaa wa kuwalea.

Watoto hao wawili huwa wanarandaranda mitaani na wakibahatika wakati mwingine hupatana na msamaria mwema anayewasaidia na chakula. Jirani mmoja aliguswa sana na hali ya watoto hao na kujaribu kuwalinda ili kuwasaidia kupata chakula.

“Tunawafahamu watoto hawa kwa sababu sisi ni majirani na kila mara tunajaribu tuwezavyo kuwasaidia kwa vyovyote tuwezavyo,” Safari alisema.

Maoni ya wanamtandao

Kisa hicho kiliwagusa wanamtandao wengi waliowahurumia watoto hao na kuwatakia heri njema.

@elicatshaka1979: "Natamani ningeweza kuwasili wote wawili, niko Afrika Kusini. La sivyo Mungu awazunguke kwa neema na ulinzi wake ili kweli wapate msaada kutoka kwa watu wanaomcha Mungu, ambao hawatanyanyasa au kuwadhulumu."

"Tafadhali Mungu akutumie kuwasaidia na kuwaondoa huko, kwa sababu si salama kwao kukaa peke yao."

@jlawrence1835: "Naomba upate msaada kwa watoto hawa wenye watu wanaowajali kwa dhati na wasiotaka kujinufaisha na kuwanyanyasa kwa msaada uliopata kupewa Mwenyezi Mungu aendelee kukubariki. safari yako ukiwasaidia wale wenye mahitaji makubwa."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live