Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama aliyeua watoto wake ili kumfurahisha mpenzi mpya, atupwa jela miaka 17

CRIME SCENE.png Mama aliyeua watoto wake ili kumfurahisha mpenzi mpya, atupwa jela miaka 17

Mon, 27 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Flossy Cherono mwenye umri wa miaka 34 alishtakiwa katika mahakama ya Eldoret kwa tuhuma za kuwaua watoto wake wawili ili kumshawishi mpenzi wake mpya kumuoa.

Aliwaua watoto wake Ivy Chelagat mwenye umri wa miaka 11 na Beryl Chepchumba mwenye umri wa miaka saba kwa kutumia panga.

Akiwa mbele ya Hakimu Reuben Nyakundi, Bi Cherono alikiri kutupa miili ya wawili hao kwenye choo cha shimo.

Mahakama ilisikia kwamba mshtakiwa aliwaua watoto hao usiku wa Julai 9, 2019 nyumbani kwao Kaburwo kaunti ya Nandi.

Upande wa mashtaka uliambia mahakama kuwa tukio hilo lilikuwa la kuogofya na mshtakiwa alistahili adhabu kali kwa kukatisha maisha ya wasichana wasio na hatia, jarida moja la humu nchini liliripoti.

Hakimu Nyakundi pia alisema alishangazwa na ungamo la mama huyo ambaye aliambia mahakama kwamba aliwaua watoto wasio na hatia ili kulinda ndoa yake.

Ripoti ya uchunguzi wa maiti kutoka Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi (MTRH) ilithibitisha kwamba watoto hao walikuwa wamenyongwa hadi kufa kabla ya kukatwa vipande vipande kwa kutumia panga.

"Watoto hao walikuwa wamenyongwa hadi kufa huku mwingine akitokwa na damu hadi kufa kutokana na jeraha kubwa kichwani," ilisema ripoti ya uchunguzi wa maiti.

Bi Cherono ana siku 14 kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live