Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama aliyekuwa amenasiwa na jembe kichwani afariki dunia

Hospitali Ya Kenyatta Mama aliyekuwa amenasiwa na jembe kichwani afariki dunia

Wed, 12 Oct 2022 Chanzo: BBC

Mama ya mtoto wa miaka miwili aliyelazwa hospitali kubwa ya rufaa ya Kenyatta jijini Nairobi ili kufanyiwa upasuaji wa kutoa jembe lililokuwa limesakama kwenye fuvu la kichwa chake amethibitisha kuwa amefariki.

Juhudi za madaktari wa Kenyatta jijini Nairobi kuokoa maisha ya mtoto huyo hazikufaulu.

Haya yanajiri kufuatia malalamiko ya umma yaliotolewa mitandaoni kwamba mtoto huyo alikosa kupokea matibabu katika Hospitali hiyo ya Kitaifa ya Kenyatta, zaidi ya saa 24 baada ya kuhamishwa kutoka hopitali nyengine ya serikali.

Katika taarifa yake hospitali hiyo ya Kenyatta imefafanua kwamba mtoto huyo alikuwa amepoteza damu nyingi na hali yake ilihitajika kuimarika kabla ya kufanyiwa upasuaji.

Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta ndiyo hospitali kuu ya umma nchini kenya, lakini mara nyingi imeshutumiwa kwa uhaba wa vifaa muhimu vya madaktari kutumia kuwahudumia wagonjwa Pamoja na kuchelewa kutoa huduma.

Bado haijabainika jinsi mtoto huyo mdogo alivyopata jeraha hilo la jembe kwenye fuvu la kichwa chake.

Chanzo: BBC