Hakuna mzazi mwenye upendo anayetumaini na kusali kupata mtoto mwenye ulemavu wa kimwili au kiakili anapozaliwa.
Matukio ya kusikitisha yanapotokea, wanandoa wanahitaji kushikamana ili kupeana upendo na utegemezo.
Mama mmoja ameeleza kisa chake cha kukataliwa na mumewe baada ya kujifungua mtoto mwenye matatizo ya kimwili.
"Ninaishi na mwanangu, Derrick, ambaye ana ugonjwa wa mishipa ya fahamu ambao umemfanya awe na kifafa. Pia ninaishi na mjukuu wangu wa kike mwenye umri wa miaka mitano anayeishi na ugonjwa wa kupooza kwa ubongo," alisema.
Derrick, kifungua mimba wake, ndiyo sababu aliacha ndoa yake baada ya baba yake kumkataa kwa kufuatia hali yake. Licha ya changamoto za maisha, ilimbidi ajitie moyo kwa sababu ya mtoto wake ambaye hajawahi kuwa na babake tangu azaliwe.
"Nilichukua muda mwingi kujifungua na hilo lilimuathiri mtoto wangu wakiume Derrick. Mambo hayajakuwa rahisi kwetu sisi tangu tulipotengana na mume wangu," alisimulia.
Akiwa bado anahangaika kumtunza mwanawe, akiuguza jeraha la huzuni na kukataliwa na mpenzi wake, bintiye Catherine Baraza pia alipata ujauzito.
"Alijifungua mtoto ambaye alipata jeraha la ubongo lililosababisha ugonjwa wa kupooza kwa ubongo," alisimulia.
Baba ya mtoto alimwacha Baraza, kwa vile mama yake alikuwa amekataliwa kwa uchungu na mpenzi wake.