Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama ajiua kisa wanae wamekula ndizi zake alizoficha

Bananas.jpeg Mama ajiua kisa wanae wamedokoa ndizi zake

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: Malawi24

Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Likineti Jere, ameripotiwa kujiua baada ya kukerwa na wanaye ambao wanadaiwa kumdokolea ndizi alizotunza ndani.

Mwanamke huyo Jere mkazi wa wilaya ya Dedza katika mkoa wa Central Region huko nchini Malawi anadaiwa kujiua kwa kunywa sumu ya kuulia wadudu .

Siku ya tukio alikuwa amekwenda kwenye sherehe ya harusi pamoja na mwanaye wa miaka miwili akiwa amehifadhi ndizi zake nyumbani akiacha maagizo mtu asichukue, lakini aliporudi alikuta zimepungua kitendo kilichomkasirisha.

Msemaji wa polisi katika eneo la Dedza kulipotokea mkasa huo Bw. Edward Kabango amesema mama huyo alirejea nyumbani akiwa amelewa baada ya kugundua ndizi zake zimeliwa alianza kuwasaka watoto wake huku na huko bila mafanikio na ndipo alipoamua kuingia ndani na kuchukua sumu ya kuulia wadudu na kunywa yeye pamoja na mwanaye huyo wa miaka miwili.

Msemaji huyo wa polisi Bw. Edward Kabango amesema mama huyo alifariki papo hapo huku mwanaye akikimbizwa katika hospitali ya wilaya hiyo ya Dedza ambako anaendelea kupatiwa matibabu ya kiafya na habari zinasema anaendelea vizuri.

Chanzo: Malawi24