Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama afunguka anavyokunywa mkojo wake kama pombe "Ni tamu kuliko Bia"

Bia Pombeee Mama afunguka anavyokunywa mkojo wake kama pombe "Ni tamu kuliko Bia"

Mon, 18 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Huku wengine wakisumbuliwa na uraibu wa pombe na dawa za kulevya, basi kuna wengine ambao wana uraibu wa kunywa mkojo wao. Daah! ama kweli kila soko na wazimu wake.

Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Carrie, yeye hunywa mkojo wake kana kwamba yuko kwenye shindano la unywaji wa pombe na anasema ni rahisi kwake kunywa mkojo kuliko maji.

Jinsi alivyoanza kunywa mkojo wake Carrie alibaini kuwa alianza kunywa mkojo wake na glasi moja tu asubuhi lakini sasa yeye hutumia hadi glasi tano kila siku.

Mama huyo amekuwa akinywa mkojo wake takribani miaka minne sasa. Carrie anasema pia hutumia mkojo wake kupiga mswaki kwa sababu huifanya meno yake yawe meupe na safi.

Alipoulizwa iwapo mkojo wake hunuka, Carrie alijibu kuwa harufu hutegemea na kile alichokula.

"Inategemea nakile ninachokula, mkojo wangu unanuka. Ina ladha tofauti kabisa leo kuliko ilivyokuwa miaka minne iliyopita. Ina chumvi nyakati fulani, na champeni ya plum nyakati nyingine," alikiri.

Iliripotiwa kuwa, miaka minane iliyopita, mama huyo mwenye watoto wa kike wanne aligunduliwa na kuwa na ugonjwa wa melanoma (kansa ya ngozi) na hivyo alianza kunywa mkojo wake akiwa na matumaini ya kuharakisha kupona kwake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live