Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama Sarah Obama Azikwa Nyumbani Kulingana na Desturi za Dini ya Kiislamu

0f16fb3c6624e699 Mama Sarah Obama Azikwa Nyumbani Kulingana na Desturi za Dini ya Kiislamu

Tue, 30 Mar 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Nyanyake Rais wa zamani wa Marekani Barrack Obama, Mama Sarah Obama amezikwa nyumbani kwake eneo la Kogelo kaunti ya Siaya hii leo Jumanne, Machi 30.

Mazishi ya mwendazake Mama Sarah yaliambatana na desturi za dini ya kiislamu ambapo shughuli hiyo iliendeshwa na sheikh Musa Ismail.

Kwenye hotuba ya Rais iliyosomwa na Waziri Rachel Omamo,Uhuru Kenyatta alimtaja Mama Sarah Obama kama mtu aliyejali maslahi ya kila binadamu hasa katika kuboresha maisha ya mtoto wa kike.

Sherehe ya mazishi ilihudhuriwa na watu wachache wakimemo maafisa wakuu serikalini, marafiki na familia ya mwenda zake.

Masharti ya kudhibiti msambao wa virusi vya COVID-19 yalizingatiwa hukuwa waombolezaji wachache pekee wakiruhusiwa nyumbani kwa mwendazake Mama Sarah.

Kulingana na maadili ya dini ya Kiislamu, hakuna mwanamke aliyeruhusiwa kukaribia kaburi, TUKO.co.ke ilifahamiswa kwamba marehemu alizikwa kando ya kaburi ya mumewe kama ilivyokuwa ombio lake.

Waziri wa Ulinzi Rachel Omamo aliyewasili kwa ndege rasmi ya kijeshi aaliwakilisha serikali kuu kwa jumla akiwa na ujumbe maalumu kutoka kwa Rais.

Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Gavana wa Kisumu Anyang' Nyong'o, katibu mkuu wa wizara ya habari na teknolojia Jerome Ochieng, katibu mkuu wizara ya ugatuzi Francis Owino, Gavana wa Siaya Cornel Rasanga miongoni mwa wengine.

Jambo la kushangaza ni kwamba wajumbe wote wa maeneo bunge katika eneo la Nyanza hawakuhudhuria mazishi ya mwenda zake.

Usalama uliimarishwa nyumbani kwa Mama Sarah huku Polisi wakiruhusu familia ya mwendazake na wageni wachache walioalikwa kuhudhuria mazishi hayo.

Mama Sarah Obama 99, alifariki dunia Jumatatu, Machi 28, akipokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga jijini Kisumu.

Familia yake kupitia kwa mwanawe Sayid Obama ilimsihi mwakilishi wadi wa sehemu hiyo Joseph Mboha kushawishi maafisa wa usalama kuruhu umma kuitizama mwili wa mwendazake.

"Tumepewa Ilani ya kuiruhusu familia na jamaa wa mwendazake Mama Sarah pekee kuutizama mwili, tunahisi kuhujumika kwa sababu mama alikua mtu wa watu" AliambiaTUKO.co.ke kwa njia ya simu.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke