Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama: Mume wa Osinachi alijificha kwenye kivuli cha uinjilisti

Osinachi .jpeg Osinachi Nwachukwu enzi za uhai wake akiwa na mumewe

Thu, 23 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mama wa aliyekuwa mwimbaji wa Injili nchini Nigeria, Osinachi Nwachukwu ameiambia mahakama kile kilitokea kwa binti yake wakati wa maisha yake ya ndoa na Peter Nwachukwu kabla hajafa.

Mume wa marehemu Osinachi alimnyanyasa binti yake na kusababisha kifo chake, Caroline Madu ameiambia Mahakama Kuu ya Abuja.

Kifo cha Osinachi Nwachukwu kilichotokea Aprili 2022 na kuzua ghadhabu kote nchini Nigeria baada ya familia yake kudai kuwa alikabiliwa na ukatili wa majumbani kupitia mikono ya mume wake.

Mume wa Osinachi, Peter Nwachukwu anakabiliwa na mashtaka 23 kuhusiana na mauaji ya bila kukusudia yaliyosababisha kifo cha Osnachi. Madam Madu ndiye shahidi mkuu katika kesi ya Nwachukwu, mume wa marehemu Osnachi.

Mama wa Osinachi aliangua kilio wakati akisimulia jinsi Peter alivyokwenda nyumbani kwake akijificha kwenye kivuli cha mwinjilisti. Madu anasema tangu Osnachi aolewe kwa miaka 14, alirudi nyumbani kwake akiwa mgonjwa.

Mama huyo alitoa ushahidi mbele ya mahakama akisema Peter hakumruhusu kumtembelea binti yake kwa sababu anamwita mchawi. Pia, hakumruhusu mwimbaji marehemu Osinachi kuchangamana na ndugu yake yeyote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live