Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mali yapeleka tena majeshi katika maeneo yanayokaliwa na waasi

Mali Yapeleka Tena Majeshi Katika Maeneo Yanayokaliwa Na Waasi Mali yapeleka tena majeshi katika maeneo yanayokaliwa na waasi

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Jeshi la Mali siku ya Jumatatu lilianza tena kupeleka wanajeshi katika ngome ya waasi huko Kidal kaskazini, maafisa wawili wa usalama walisema, huku mapigano yakizuka tena hivi karibuni katika eneo hilo.

"Ikiwa ni sehemu ya kupanga upya mipango yetu katika eneo la kaskazini, tumeanza kupeleka vikosi vyetu eneo la kaskazini mashariki mwa Kidal," afisa wa jeshi wa Mali ambaye alizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, aliliambia shirika la habari la AFP.

Msafara uliondoka Jumatatu asubuhi katika mji wa Gao ulioko Kaskazini, takriban kilomita 300 Kusini Magharibi mwa Kidal, , chanzo hicho kiliongeza.

Afisa mwingine wa usalama alisema, msafara huo ulikuwa na magari 119 na kwa sasa yamesimamishwa kwenye barabara inayoelekea kaskazini mwa Gao.

Wakuu wa usalama wa taifa walifanya uamuzi wa kuyatuma majeshi hayo katika mkutano wa Jumapili jioni, aliongeza.

Eneo la Kaskazini mwa Mali linashuhudia kuanza tena kwa uhasama kati ya makundi yanayotaka kujitenga, ya wa Tuareg wanaotaka kujitenga, na ongezeko kubwa la mashambulizi ya wanajihadi dhidi ya jeshi la Mali tangu mwisho mwa mwezi Agosti.

Mwaka 2012, watu wa kabila la Tuareg lililoko Kaskazini mwa Mali walisimama na kuungana na kundi la Waislamu wenye msimamo mkali la Ansar Dine.

Maeneo ya nchi hiyo vikiwemo vituo vitatu vya kaskazini vya Gao, Kidal na Timbuktu yameangukia mikononi mwa Wanajihadi.

Kuongezeka kwa ghasia za hivi karibuni kunatokana na hatua inayoendelea ya kuondolewa kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kuleta utulivu cha MINUSMA, ambacho kimetakiwa kuondoka na utawala wa kijeshi.

Chanzo: Bbc