Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mali yaendeleza shutuma dhidi ya Ufaransa

118678269 Goita Mali yaendeleza shutuma dhidi ya Ufaransa

Wed, 19 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mambo ya nje wa Mali, Abdoulaye Diop amesema serikali ya kijeshi ya nchi hiyo itatumia haki yake ya kujilinda ikiwa Ufaransa itaendelea kudhoofisha uhuru na usalama wa taifa hilo la Afrika Magharibi.

Diop, ameyasema hayo jijini New York katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kurejelea madai kwamba Ufaransa ilikiuka mipaka yake ya anga na kukabidhi silaha kwa Wanamgambo wa Kiislamu ambao wanaendesha mashambulizi kaskazini mwa Mali kwa muongo mmoja sasa.

Amesema, “Ipo haja ya kuwa na mkutano maalum wa Baraza la Usalama ambao utatoa mwanga kuhusu ushahidi wa vitendo vya udadisi, ujasusi na uharibifu vinavyofanywa na Ufaransa, sisi Mali tutatumia haki yetu ya kujilinda ikiwa Ufaransa itaendelea kudhoofisha uhuru na usalama wa taifa letu.”

Hata hivyo, Mamlaka za usalama na Serikali ya nchini Ufaransa zimekuwa zikikanusha shutuma hizo, wakati ambapo uhusiano wake na Mali umeendelea kudorora tangu mapinduzi ya Agosti mwaka 2020 na baada ya kuwaondoa askari wake, waliotumwa mwaka 2013 kusaidia kupambana na uasi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live