Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mali na Guinea yaonja hasira za ECOWAS

Mali ECOWAS Mali na Guinea yaonja hasira za ECOWAS

Sat, 5 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika mkutano huo wa jana viongozi wa kanda hiyo walijizuia kuiwekea vikwazo Burkina Fasso na badala yake kuwataka watawala wa kijeshi kutangaza tarehe rasmi ya kurejea kwa utawala wa kiraia.

Kadhilika imetaka kuachiwa huru kwa viongozi wote wa kisiasa wanaoshikiliwa ikiwemo rais Roch Christian Kabore.

Ingawa ECOWAS imetishia kuichukulia vikwazo Burkina Fasso iwapo wanajeshi hawatarejesha utawala wa kiraia, hatua kama hizo hazijafanikiwa sana kwa mataifa ya Mali na Guinea.

Licha ya juhudi za kutaka kurejeshwa utawala wa kiraia nchini Mali, watawala wa kijeshi walipuuza ratiba ya kufanyika uchaguzi wa kidemokrasia mwezi huu na badala yake wamependekeza mchakato huo kuchukua hadi miaka mitanoo.

Uamuzi huo ulijibiwa vikali na ECOWAS iliyotangaza vikwazo dhidi ya Mali ikiwemo kufunga mipaka ya nchi zake na taifa hilo lenye mzozo.

Hatma ya kurejea utawala wa kiraia nchini Guinea nayo bado inajikokota. ECOWAS hapo jana ilitangaza vikwazo ziada kwa mataifa hayo mawili ikiwemo dhidi ya viongozi wa kijeshi na familia zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live