Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mali : Wanajeshi wa MINUSMA wameanza kuondoka

Minusma Un Un Mali : Wanajeshi wa MINUSMA wameanza kuondoka

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wameripotiwa kuondoka katika kambi ya Kidal kaskazini mwa Mali, eneo ambalo linakabiliwa na utovu wa usalama.

Kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwaka wa 2020, uongozi mpya wa kijeshi nchini Mali mwezi Juni, uliwataka wanajeshi wa UN kuondoka kwa tuhuma za kushindwa katika majukumu yao.

Wanajeshi wa UN (MINUSMA) nchini Mali wamekuwa wakipambana na makundi ya watu wenye silaha ambapo maofisa wake 180 wameripotiwa kuuawaua.

MINUSMA imekuwa na wanajeshi karibia 15,000 katika taifa hilo la Afrika ambalo linakabiliwa na changamoto za kuisalama.

Kujiondoa kwa MINUSMA kumeamsha makabiliano kati ya makundi pinzani yenye silaha kaskazini mwa Mali na serikali ya kijeshi

Kwa mujibu wa makubaliano, wanajeshi wa Umoja wa Mataifa walitakiwa kuwa wameondoka katika taifa hilo la Afrika Magharibi kufikia mwishoni mwa mwaka huu japokuwa walianza kujiondoa kwenye kambi zao mapema mwezi Julai.

Kujiondoa kwa MINUSMA kumeamsha makabiliano kati ya makundi pinzani yenye silaha kaskazini mwa Mali na serikali ya kijeshi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live