Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mali: Walinda amani waondokoka kambi ya Tessalit

Somalia Somalia AU Mali: Walinda amani waondokoka kambi ya Tessalit

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Mataifa, hapo jana umesema wanajeshi wake wa kulinda amani walilazimika kuondoka kwa dharura kwenye kambi yao ya Tessalit, kaskazini mwa nchi ya Mali, kwa kile kimedaiwa kuwa usalama wao ulikuwa hatarini.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la Mali kupitia ukurasa wake wa kijamii wa X zamani Twitter, vikosi vyake vilichukua usimamizi wa kambi hiyo siku ya Jumamosi, ikiwa ni makabidhiano ya kwanza kwenye mkoa wa Kidal ambako kunashuhudiwa mapigano.

Kuondoka kwa wanajeshi wa umoja wa Mataifa nchini humo baada ya karibu miaka 13, kumeibua hofu ya usalama, hasa wakati huu ambapo makundi ya waasi kaskazini mwa nchi hiyo, yakichukua tena silaha kupigana na jeshi.

Tume ya MINUSMA kwenye taarifa yake imesema kuwa, ililazimika kuwaondoa haraka wanajeshi wake kwenye kambi ya Tessalit, baada ya kupokea taarifa ya uwezekano wa vikosi hivyo kushambuliwa, ambapo kwa saa kadhaa wafanyakazi wake walilazimika kujificha katika mahandaki.

Msafara wa wanajeshi hao ulielekea kwenye mji wa Gao, tayari kwa maandalizi ya kuondoka kabisa nchini humo, baada ya agizo la utawala wa Kijeshi mwezi juni, ambao ulitaka vikosi hivyo kuondoka ifikapo Desemba mwaka huu.

Kujiondoa kwa takriban wanajeshi 11,600 na maafisa wa polisi 1,500 kunafaa kuendelea hadi Desemba 31, na kumezidisha uhasama kati ya vikundi vilivyojihami vilivyopo kaskazini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live