Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mali: Walinda amani wa UN wamekabidhi kambi kwa serikali

Mali Mali Walind Aamani Tikmbukyutu.png Mali: Walinda amani wa UN wamekabidhi kambi ya Timbuktu kwa serikali

Sat, 30 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchini Mali, ujumbe wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa maarufu kama (Minusma) umesema unakabidhi moja ya vituo vyake kuu vya mwisho katika eneo la kaskazini la Timbuktu kwa mamlaka kwenye taifa hilo.

Awali ujumbe huo ulikuwa umeratibiwa kukabidhi kambi zake katika eneo la Gao na Timbuktu kwa mamlaka ya Mali mwezi Januari.

Kutokana na hali ya usalama inayoendelea kuwa mbaya katika eneo hilo linalokabiliwa na makundi ya kijihadi, imesababisha kuondoka mapema kwa vikosi hivyo kutoka katika mji wa Timbuktu.

Jeshi la Mali lilitoa wito kwa walinda amani wa MINUSMA kuondoka mara moja kwenye taifa hilo mwezi Juni, uhusiano kati ya pande hizo mbili ukiendelea kupungua.

MINUSMA iliripoti kuwapoteza karibia maofisa wake 180 katika kipindi cha miaka kumi wakati ilipokuwa ikijaribu kurejesha usalama katika nchi hiyo ya Sahel inayokabiliwa na changamoto za kuisalama kutoka kwa makundi ya kijihadi.

Baraza la usalama katika Umoja wa Mataifa lilipiga kura kuidhinisha kumalizika kwa ujumbe huo wa walinda amani karibia elfu 15 wa UN tarehe 30 ya mwezi Juni na kuutaka kuwa umeondoka kufikia tarehe 31 ya mwezi huu wa Desemba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live