Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mali: Waasi wa Tuareg wakanusha kuwepo kwa kaburi la pamoja

Mali Waasii Waaasi.png Mali: Waasi wa Tuareg wakanusha kuwepo kwa kaburi la pamoja Kidal

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waasi wa Tuareg wanaotaka kujitenga wamekanusha kuwepo kwa kaburi la umati ambalo jeshi la Mali lilidai kugundua wiki iliyopita huko Kidal (kaskazini), mji ambao ni ngome ya waasi uliotekwa tena na vikosi vya jeshi la serikali na washirika wake.

"Madai" haya, "yaliyotengenezwa", ni "upotoshaji tupu ambao kwa hakika unakusudiwa kuficha ukweli kuhusiana na mauaji ya kutisha yaliyofanywa na makundi mawili ya kigaidi Wagner-FAMa (vikosi vya jeshi la Mali)", waasi wanaotaka kujitenga wamesema katika taarifa.

"Katika jimbola Kidal, hakuna madai yoyote, hata kwa njia ya uvumi, ambayo yamewahi kuripotiwa na chanzo chochote kinachohusiana na ukiukwaji wa haki za binadamu unaohusishwa na vikosi vya CSP-PSD," muungano wa makundi yenye silaha, wameongeza. Wanalaani "ujanja mbaya wa kupuuza mauaji yote yanayofanywa" na wanajeshi wa Mali na washirika wao kutoka kundi la wanamgambo wa Urusi la Wagner, ambao utawala wa kijeshi unakanusha uwepo wake.

Jeshi la Mali lilidai kugundua kaburi hili la umati mnamo Novemba 16 wakati wa operesheni za usalama. "Kaburi hili la umati ni ukumbusho wa ukatili unaofanywa na magaidi wasio na sheria," jeshi lilisema, bila maelezo zaidi.

Baada ya miaka minane ya utulivu, uhasama ulianza tena mwezi Agosti kaskazini mwa Mali kati ya vikosi vya serikali na waasi wanaotaka kujitenga. Kujiondoa kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa, uliossababisha waasi na jeshi kupigana kwa lengo la kudhibiti eneo la Kidal, mamlaka kuu ikitaka kurejeshwa kwa kambi, waasi wanapinga. Kutekwa tena katikati ya Novemba na jeshi la Kidal, ngome ya madai ya uhuru, ni mafanikio ya mfano kwa wanajeshi ambao walichukua madaraka kwa nguvu mnamo 2020.

Katika kivuli cha mapigano ya ardhini, kambi hizo mbili pia zinakabiliana kwenye mitandao ya kijamii, hasa X (zamani ikiitwa Twitter), TikTok na Facebook, kupitia kurasa za uuungwaji mkono, ambazo nyingi ziliundwa hivi majuzi, dhidi ya habari potofu. "Kila upande unatoa toleo lake la kile kinachotokea na kudharau kile cha adui, ambacho kinawasilisha kama propaganda," Seidik Abba, mwandishi wa habari wa Niger na mchambuzi wa kisiasa aliyebobea katika Sahel, aliliambia shirika la habari la AFP hivi karibuni.

Utawala wa kijeshi ulivunja ushirikiano wa kihistoria wa kijeshi na Ufaransa na washirika wake wa Ulaya na hivyo kuanzisha uhusiano na Urusi na kuamuru ujumbe wa Umoja wa Mataifa kuondoka. Baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa kutoka kambi ya Gossi, katikati mwa Mali, jeshi la Mali pia lilitangaza kwamba limegundua "kaburi la watu wengi" mnamo 2022. Jeshi la Ufaransa lilishutumu mara moja udanganyifu, na kutoa picha za ndege zisizo na rubani zinazoonyesha mamluki wakizika miili siku chache kabla, kulingana na jeshi la Ufaransa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live