Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mali: Utawala wa kijeshi wapeleka mbele mchakato kura za maoni

Mali Putin Mazungumz Mali: Utawala wa kijeshi wapeleka mbele mchakato kura za maoni

Sat, 11 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya kijeshi nchini Mali imetangaza kuakhirishwa tarehe ya kufanyika kura ya maoni ya katiba katika nchi hiyo ya Kiafrika.

Mali inatawaliwa na serikali ya kijeshi kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2020 na 2021. Serikali ya kijeshi ya Mali jana ilitangaza kuakhirisha kura ya maoni ya katiba iliyopangwa kufanyika Machi 19, ikitoa hakikisho kwamba itaheshimu ahadi yake ya kurejesha uongozi wa nchi kwa raia mwaka 2024.

Msemaji wa serikali Kanali Abdullah Maiga, alitangaza katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba, tarehe ya kura ya maoni iliyopangwa itaakhirishwa kwa kusogezwa mbele kidogo. Kura hiyo ya maoni ni hatua ya kwanza ikifuatiwa na zoezi la upigaji kura katika uchaguzi wa Februari 2024 vitakavyohakikisha utawala wa kiraia unarejea madarakani nchini Mali.

Maiga ameongeza kuwa: sababu ya serikali ya kijeshi kuakhirisha zoezi hilo ni kuhakikisha makarani wa tume ya kuendesha uchaguzi wanasambazwa katika mikoa yote nchini na kutaka rasimu ya katiba mpya ipate maoni ya wananchi wote.

Tarehe mpya ya kura ya maoni inatakiwa kuainishwa baada ya kushauriana na mamlaka huru ya uendeshaji uchaguzi na wote wanaohusika katika mchakato wa uchaguzi wenyewe.

Katiba hiyo mpya ni kipengele muhimu cha mpango mkubwa wa mageuzi ambao jeshi limekusudia kuyaleta na kuyatumia kuhalalisha kuendelea kuongoza nchi hadi 2024, kwa ajili ya kukabiliana na kushamiri kwa mielekeo ya kufurutu mpaka na mgogoro mkubwa wa pande kadhaa ulioikumba Mali.

Mali imekumbwa na wimbi la hujuma za makundi yenye itikadi kali na mielekeo ya kufurutu mpaka pamoja na machafuko ya kila aina tangu mwaka 2012.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live