Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mali: Uongozi wa kijeshi wasitisha mkataba wa amani wa 2015

Mali Waasii Waaasi.png Mali: Uongozi wa kijeshi wasitisha mkataba wa amani wa 2015

Fri, 26 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa kijeshi nchini Mali, umetangaza kusitisha mara moja, mkataba muhimu wa amani wa 2015, uliosainiwa na makundi ya waasi kaskazini mwa nchi hiyo baada ya kushuhudiwa makabliano ya miezi kadhaa kati ya jeshi la na waasi wa kaskazini mwa nchi hiyo.

Msemaji wa serikali, Abdoulaye Maiga, amesema hatua hiyo imetokana na baadhi ya makundi yaliosaini mkataba huo kubadili msimamo lakini pia kile ametaja kuwa vitendo vya uadui kutoka kwa mpatanishi mkuu Algeria.

Algeria imekuwa mpatanishi mkuu katika jitihada za kurejesha amani nchini Mali, kufuatia makubaliano ya amani ya 2015 kati ya serikali na makundi yenye silaha ya Tuareg, makubaliano ambayo wachambuzi wengi waliitazama kuwa ya muhimu katika kuleta amani nchini Mali.

Hata hivyo makubaliano hayo yaliingia doa mwaka uliopita, wakati mapigano yalizuka kati ya waasi hao na vikosi vya serikali baada ya kushuhudiwa utulivu wa miaka minane, pande zote zikinga’ang’ania kujaza pengo lililoachwa na walinda amani wa umoja wa mataifa.

Hata kabla ya tangazo hili, waasi hao chini ya mwavuli wa Coordination of Azawad Movements (CMA), mnamo julai 2022 waliishtumu utawala wa kijeshi uliochukua madaraka 2020 kwa kutoonesha nia ya kutekeleza mkataba huo wa amani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live