Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mali, Tunisia zatakata fainali Afcon 2021

4643b3bf579940dcf68e676418602ad6 Mali, Tunisia zatakata fainali Afcon 2021

Thu, 19 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MALI imejihakikishia nafasi ya kukaribia kucheza kwa mara ya nane mfululizo fainali ya Mataifa ya Afrika, Afcon 2021, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji Namibia.

Kwa ushindi huo, Mali imefikisha pointi 10 na kuongoza Kundi A na kujihakikishia nafasi ya kucheza hatua inayofuata ya michuano hiyo, huku Guinea ikiwa katika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi nane na Namibia ina pointi tatu.

Mabao yote matatu ya Kundi A yalipatikana katika dakika 40 za mwanzo za mchezo huo wakati penalti ya Mali ikiokolewa katika kipindi cha pili na mashuti ya wachezaji wa Namibia yakigonga mwamba.

Sekou Koita wa Red Bull Salzburg aliifungia Mali bao dakika ya 12 baada ya kuukokota mpira katika eneo la hatari na kupiga shuti lililompita kipa Virgil Vries na kuingia pembeni ya goli.

Tanzania 1-1 Tunisia (Kundi J)

Tunisia wamepata nafasi ya kufuzu kwa hatua inayofuata licha ya kubanwa na Taifa Stars ya Tanzania baada ya kufungana bao 1-1 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam juzi usiku.

Wageni Tunisia walitawala mchezo huo katika kipindi cha kwanza na kupata bao la kuongoza dakika 11 tangu mchezo huo kuanza kwa bao la Seifeddine Khaoui anayeichezea Marseille ya Ufaransa.

Taifa Stars ilipambana huku ikionekana kama Tunisia wangeshinda kirahisi mchezo huo, lakini mchezaji aliyeingia akitokea benchi Feisal Salum alifunga bao la kusawazisha kwa shuti kali la mbali lililoifanya Tanzania kuondoka na pointi moja.

Sare hiyo ilitosha kuiwezesha Tunisia kupata nafasi ya kwenda Cameroon baada ya kujihakikishia nafasi ya kumaliza katika nafasi mbili za kwanza kutoka katika Kundi J, shukrani kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania katika mchezo wa kwanza nchini Tunisia Jumanne ya wiki iliyopita.

Kwa matokeo hayo, Tanzania ipo katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi mbili nyuma ya Guinea ya Ikweta iliyopo katika nafasi ya pili, huku Libya nayo ikiendelea kuwa nafasi ya kufuzu licha ya kuwa mkiani mwa msimamo ikiwa na pointi tatu.

Sudan 1-0 Ghana (Kundi C)

Sudan ilifunga bao la dakika za mwisho na kuipatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ghana katika mchezo wa Kundi C juzi.

Matokeo hayo yana maana kuwa Ghana inabidi kuendelea kusubiri kufuzu kwa fainali hizo wakati ilipouanza mchezo huo ikijua kuwa sare tu ingetishia nafasi yake ya kufuzu lakini mambo hayakuwa hivyo.

Timu nyingine katika kundi hilo ni Sao Tome ambayo haina hata pointi moja baada ya kuchapwa 4-2 kwa Afrika Kusini katika mchezo wa Jumatatu.

Afrika ya Kati 0-2 Morocco (Kundi E)

Morocco imeendeleza kutofungwa katika Kundi E baada ya kushinda 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati katika mchezo uliopigwa katika jiji la Cameroon la Douala kwa sababu Bangui hakuna uwanja mzuri.

Mchezaji wa Chelsea, Hakim Ziyech alifunga dakika sita kabla ya mapumziko baada ya kupiga mpira wa adhabu.

Ziyech baadae alichangia kupatikana kwa bao la pili lililofungwa katika muda wa majeruhi wakati alipotoa pasi ya mwisho kwa Youssef En Neysri aliyeujaza wavuni.

Matokeo hayo yana maana kuwa Morocco wako kileleni katika kundi lao wakiwa na pointi 10 na wanahitaji sare tu kutoka katika mechi mbili za mwisho ili kufuzu kwa fainali.

Sierra Leone 0-0 Nigeria,

Lesotho 0-0 Benin (Kundi L)

Mechi mbili za Jumanne katika Kundi L zilishindwa kutoa washindi wakati Nigeria kwa mara nyingine tena walipobanwa na Sierra Leone.

Leone Stars iliyokuwa nyuma kwa mabao 4-0, ilipambana na kulazimisha sare ya 4-4 dhidi ya vigogo wa soka la Afrika, Nigeria.

Licha ya matokeo hayo, Super Eagles inaweza kufuzu endapo itapata ushindi katika mchezo utakaofanyika Freetown, Sierra Leone.

Matokeo hayo yanaifanya Nigeria kuendelea kuongoza katika kundi lake ikiwa na pointi nane ikiwa ni moja zaidi ya Benini iliyopo katika nafasi ya pili.

Togo 1-3 Misri (Kundi G)

Misri wamepanda juu ya Comoro kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa baada ya kushinda 3-1 dhidi ya Togo ambayo kwa sasa haipo tena katika mbio za kuwania kufuzu.

Mabao ya Mapharaoh yalifungwa katika dakika ya 18 na Mohamed Magdi wakati lile la pili lilipatikana baada ya nusu saa na Djene Dakonam na la tatu likifungwa na Trezeguet katika dakika ya 52.

Bao la Togo la kufutia machozi lilitokana na kona ambayo haikuokolewa vizuri na kumuwezesha Elom Nya-Vedji kufunga.

Matokeo hayo yana maana kuwa Misri na Comoro zote kila moja ina pointi nane na zote zina nafasi ya kufuzu.

Kenya ambayo ilichapwa 2-1 huko Comoro Jumapili ina pointi tatu na ni timu pekee ambayo inaweza kufuzu kutoka katika kundi hilo huku ikibakiza mechi mbili dhidi ya Misri na Togo.

Chanzo: habarileo.co.tz