Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mali: Tuna ushahidi, Ufaransa inashirikiana na magaidi

Waaizriirir Mali Ufaransa Mali: Tuna ushahidi, Ufaransa inashirikiana na magaidi

Wed, 8 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa Mali, Choguel Kokalla Maïga, amefichua - katika mahojiano maalumu na televisheni ya Al-Jazeera ya Qatar- kuwa Bamako ina taarifa sahihi na ushahidi kwamba baadhi ya magaidi waliko nchini Mali wamekuwa wakiwasiliana na Ufaransa.

Maiga ameeleza kuwa: “Mali haikutaka kukata ushirikiano wake na Ufaransa bali Paris ilitaka kutulazimisha matakwa na maamuzi yake hapa nchini, na tukawaambia kuwa zama hizo zimepita, hivyo tunachagua washirika wetu na kuchagua tunachotaka kufanya.” Amesema kwamba Wafaransa waliamua kuondoka Mali baada ya ujio wa serikali ambayo hawakuipenda.

Waziri Mkuu wa Mali amesema kwamba "Wafaransa waliamini kwamba tutawasihi kubakisha majeshi yao katika nchi yetu, lakini hatukujali hatua hiyo," na "tulipoijulisha Paris kwamba tumekataa maagizo yake, iliamua kujiondoa katika mikataba ya ushirikiano wa pande mbili na kuondoa majeshii yake katika ardhi ya Mali."

Maiga amesisitiza kuwa kipaumbele cha Taifa la Mali ni kuimarisha usalama na amani, na kwamba wakati wa uwepo wa wanajeshi wa Ufaransa nchini humo, ugaidi haukutokomezwa na kwamba serikali ya Mali haikuweza kudhibiti tena maeneo yote ya nchi.

Waziri Mkuu wa Mali ametoa wito kwa serikali ya Ufaransa kubadili mienendo yake kuhusiana na watu wa Afrika.

Ufaransa ilitangaza kuwaondoa wanajeshi wake nchini Mali mwezi wa Agosti mwaka jana, na hivyo kumaliza operesheni yake ya kijeshi katika nchi hiyo ya Kiafrika baada ya kuwepo kwa miaka 9 katika kalibu ya kikosi cha kijeshi cha Barkhane.

Uamuzi huo wa Paris ulichukuliwa baada ya kuibuka mivutano katika uhusiano baina ya baraza tawala la kijeshi la Mali na serikali ya Ufaransa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live