Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mali: Kambi ya kijeshi yashambuliwa na magaidi

Jeshi Mali.jpeg Mali: Kambi ya kijeshi yashambuliwa na magaidi

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchini Mali, kijiji cha Kouakourou kilicho katika jimbo la Mopti kilikumbwa na mashambulizi ya makundi ya kigaidi ya Katiba Macina na kundi linalotetea Uislamu na Waislamu jioni ya Jumatano Agosti 7, kulingana na vyanzo vya ndani. Kambi ya wanajeshi wa Mali ililengwa katika shambulio hili ambalo lilisababisha majeruhi kadhaa.

Siku ya Alhamisi hii, Agosti 8, wakazi wa kijiji cha Kouakourou, katikati mwa Mali, waliamka kwa hofu na wasiwasi, kimesema chanzo cha eneo hilo. Siku moja kabla, Agosti 7, karibu 1:00 usiku., watu wenye silaha waliingia katika kijiji hiki kwa pikipiki. Waliekea kwenye kikosi cha kijeshi kilichowekwa karibu na Mto Niger. Majibizano makali ya risasi yalianza, vikosi vya usalama vilipambana, lakini vililazimika kurudi nyuma dhidi ya washambuliaji. Magaidi hao walichukuwa udhibiti wa kituo cha jeshi. Vifaa vya jeshi viliporwa na kituo hicho kilichomwa.

Wakati wote wa shambulio hilo, wakaazi walijificha kwenye nyumba zao. Mnamo Julai 2023, shambulio la bomu lililotegwa katika gari lilifanyika katika hali kama hiyo, na kuua askari kadhaa na kuwajeruhi wakaazi. Jimbo la Mopti mara nyingi hulengwa na magaidi

Kouakourou ni ishara ya kijiji na shahidi wa mgogoro katikati mwa Mali. Mnamo mwaka wa 2017, ilikuwa moja ya vijiji vya kwanza katika jimbo hilo kuwekewa vikwazo kwa miezi kadhaa. Wakazi waliokataa kufuata sheria mbaya za makundi ya kigaidi. Tangu wakati huo, kambi ya kijeshi imeanzishwa katika kijiji kwa ombi la wakazi. Licha ya uharibifu huo wa siku ya Jumatano Agosti 7, vikosi vya ulinzi vya Mali vilirejesha udhibiti wake katika kambi hiyo.

Kaskazini zaidi, katika jimbo la Kidal, wanajeshi wa Mali wametangaza kuwa wamefanikiwa kufanya mashambulizi ya mabaya kwenye maeneo ya magaidi siku ya Jumatatu hii, Agosti 5. Magaidi waliangamizwa na kambi na magari kuharibiwa, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live