Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mali:Jeshi laita makundi yenye silaha kuzungumza

Jeshi Jeshii Mali Mali.png Mali:Jeshi laita makundi yenye silaha kuzungumza

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Mali siku ya Jumatatu imetoa wito kwa makundi yenye silaha kaskazini mwa nchi ambayo yametia saini makubaliano ya amani yaliyokwama, kufanya upya mazungumzo, huku hofu ya kuzuka upya kwa mapigano ikiongezeka kutokana na kujiondoa kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa.

Wito huu ulipotolewa, msemaji wa shirika linalounganisha makundi haya ameshutumu ndege za jeshi la Mali kwa kushambulia kwa mabomu ngome za Uratibu wa mavuguvugu ya Azawad (CMA), kundi lenye idadi kubwa ya Watuareg lililotia saini kwenye makubaliano hayo, katika eneo la Kidal, bila kufanya uharibifu wowote.

Mvutano umekuwa ukiongezeka kwa miezi kadhaa kati ya serikali kuu na makundi husika. Mvutano huo umeongezeka baada ya kujiondoa kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliotumwa nchini Mali tangu 2013, hatua iliyochukuliwa na mamlaka ya Mali.

Makundi yenye silaha yanapinga kukabidhiwa kwa kambi za ujumbe huo kwa jeshi la Mali, huku kukiwa na ushindani wa kudhibiti maeneo mbalimbali ya Mali.

Mvutano huu ulifikia kilele kwa uhamisho wa kambi ya Umoja wa Mataifa kutoka Ber katikati ya mwezi Agosti, ambayo ilisababisha mapigano kati ya askari na wanajihadi, lakini pia kwa vitendo vya uhasama kati ya jeshi na CMA.

Hali hiyo inazusha hofu kwa mustakabali wa makubaliano ya mwaka 2015 yanayozingatiwa kuwa muhimu kwa utulivu wa nchi ya Sahel iliyokumbwa na machafuko tangu kuzuka kwa waasi wanaotaka kujitenga na Wasalafi kaskazini mwaka wa 2012.

Mkataba huo unaoitwa Algiers Accord ulitiwa saini na CMA, na makundi yenye silaha yanayoiunga mkono serikali na serikali ya Mali. Wanajihadi wanaendelea kupambana na serikali chini ya bendera ya Al-Qaeda au kundi la Islamic State.

Wasiwasi wa mustakabali wa makubaliano hayo ulionyeshwa kwa wingi Jumatatu wakati wa kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali El Ghassim Wane alibainisha "kuzorota kwa miundo ya ufuatiliaji" ya makubaliano.

Balozi wa Marekani Linda Thomas-Greenfield amesema "amesikitishwa" na mapigano yaliyotokea Ber na "kuanzishwa kwa mapigano kaskazini".

"Ikiwa vita vitazuka, vitasababisha uharibifu usioweza kuelezeka, usiofikirika kwa Wamali," amesema.

Nchi kadhaa zimetoa wito wa kuanzishwa tena kwa mazungumzo.

Katika taarifa iliyotolewa wakati huo huo, Waziri wa Maridhiano wa Mali, anayesimamia makubaliano ya amani, Kanali Meja Ismaël Wagué, amesema "kualika" vuguvugu zilizotia saini "kurejea kwenye meza ya mazungumzo (ili) kuondokana na changamoto za sasa kupitia mazungumzo".

"Serikali inasalia kujitolea kwa makubaliano," pamoja na usitishaji mapigano uliofikiwa mwaka uliopita, amesema.

Lakini, wakati huo huo, Mohamed El Maouloud Ramadane, msemaji wa muundo unaoleta pamoja makundi yaliyotia saini tangu 2021, ameliambia shirika la habari la AFP kurushwa kwa mabomu machache kwenye maeneo ya waasi wa zamani huko Anefis, bila kusababisha uharibifu wowote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live