Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mali: Jeshi la Mali lakiri kupioteza wanajeshi wake

Jeshi Mali.jpeg Mali: Jeshi la Mali lakiri kupioteza wanajeshi wake

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya mapigano ya hivi karibuni huko Tinzaouatène, eneo hili la Mali lililo kwenye mpaka wa Algeria, jeshi la Mali limetoa taarifa mpya kwa vyombo vya habari wakati zikirikodiwa taarifa za kwanza kutoka kwa kundi lenye uhusiano uhusiano na serikali ya mali la Wagner.

Washirika hawa wawili walioko katika uwanja wa vita kaskazini mwa Mali dhidi ya waasi wa Mkakati na Mfumo wa Kudumu (CSP) wanatambua kuwa wamepoteza wanajeshi wao na hivyo kushindwa katika vita katika eneo hilo.

Nchini Mali, makao makuu ya jeshi la Mali linasema katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba wakati fulani katika mapigano, askari wake walikuwa wamezingirwa na, nanukuu, "muungano wa vikosi vya kigaidi kutoka Sahel". "Ujasiri na jitihada za askari wetu haukufanya iwezekane kuepusha idadi kubwa ya hasara kwa upande wa raia na mali," inaongezataarifa hiyo kwa vyombo vya habari.

Bamako inaongeza kuwa adui pia alitumia magari ya yaliokuwa yametegwa mabomu dhidi ya askari wake. Ghasia za mapigano hayo zimethibitishwa na vyombo vya habari rvya serikali vya Urusi ambavyo vinataja kundi la wanamgambo la Wagner na maelezo mengine. Katika uwanja wa vita, dhoruba ya mchanga iliruhusu makundi yenye silaha kuongeza idadi yao hadi wapiganaji 1,000. Ndege zisizo na rubani zilitumiwa dhidi ya wanajeshi wa Mali na wapiganaji wa Wagner.

makamanda wawili muhimu wa Urusi waliripotiwa kuuawa wakati wa mapigano hayo: Mtaalamu wa propaganda duniani kote wa Wagner na kamanda wa kijeshi wa kundi hilo anayejulikana zaidi kwa jina lake la utani la "Proud" waliangamia katika mapigano hayo. Ujumbe wake wa mwisho wa redio kabla ya kufa: "Tumebaki watatu tu, tunaendelea kupigana."

Licha ya mzozo wa wanajeshi wa FAMa na wasaidizi wao wa Wagner huko Tinzaouatène na hasara waliyoipata, John Lechner, mtafiti wa Marekani aliyebobea katika kundi la Wagner, anabaini kwamba: "hii haijadhoofisha imani ya mamlaka ya Mali kwa mamluki wa Urusi".

Alipohojiwa na RFI, amebaini kwamba "Bamako bila shaka ingependa uwekezaji zaidi kutoka Urusi katika vita dhidi ya waasi". Hali iliyotokea Tinzaouatène inapaswa kuwa fundisho kwa "kujipanga upya kwa mashambulizi na kuendeleza vita", anasema John Lechner.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live