Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mali, Guinea, Burkina Faso zaomba kurudishwa Ecowas, AU

Ecowassssssss.jpeg Mali, Guinea, Burkina Faso zaomba kurudishwa Ecowas, AU

Sat, 11 Feb 2023 Chanzo: Mwananchi

Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi tatu za Afrika Magharibi ambazo zilipitia mapinduzi ya kijeshi hivi karibuni wametaka kurejeshwa katika kambi mbili muhimu za kikanda kufuatia ziara ya mjumbe wa Russia, Sergey Lavrov katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Aljazeera, wanadiplomasia wakuu wa Mali, Guinea na Burkina Faso walieleza hayo katika taarifa yao ya pamoja Alhamisi Februari 9, 2023, kwamba wamekubaliana kufanya kazi pamoja kushinikiza kuondolewa kwa kusimamishwa kwao katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) na Umoja wa Afrika (AU).

Abdoulaye Diop wa Mali, Morissanda Kouyate wa Guinea na Olivia Rouamba wa Burkina Faso walifanya mazungumzo katika mji mkuu wa Burkina Faso kuzungumzia jambo hilo.

Nchi hizo tatu zimekubali kuunganisha juhudi zao na kufanya mipango ya pamoja ya kuondoa hatua za kusimamishwa na vikwazo vingine na Ecowas na AU, kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano huo.

Mfululizo wa mapinduzi ulifanyika katika nchi hizo tatu tangu mwaka 2020 na kuleta serikali ambazo zimekabiliana na shinikizo kutoka nje la kurejesha utawala wa kiraia na kusababisha kusimamishwa kwa vikundi vya kikanda.

Kuongezeka kwa ukosefu wa usalama katika eneo la Sahara kumesababisha mawaziri watatu kukubaliana na hoja ya kuunganisha nguvu na nchi za ukanda huo ili kukabiliana na janga hilo.

Chanzo: Mwananchi