Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malema aongoza maandamano kumtaka Museveni kuruhusu ushoga

Wet Malema Malema aongoza maandamano kuitaka Uganda kuruhusu ushoga

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa chama cha Wapigania Uchumi Huru, EFF nchini Afrika Kusini Julius Malema ameongoza maandamano ya wafuasi na wanachama wa chama hicho kuelekea ubalozi wa Uganda Nchini Afrika Kusini kupinga kitendo cha Bunge la Uganda kupitisha mswada wa sheria unaotoa adhabu kali kwa watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ikiwemo ushoga na usagaji.

Malema amemtaka Museveni kutosaini mswada huo kuwa sheria na kumtaka awaache raia wa Uganda waishi watakavyo (ikiwa ni pamoja na uhuru wa kuwa na kifaragha).

Bunge la Uganda hivi karibuni lilipitisha sheria inayoharamisha kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja (LGBTQ), na kuzipa mamlaka madaraka mapana katika kuwalenga raia wa Uganda ambao tayari wanakabiliwa na ubaguzi wa kisheria na manyanyaso wanayofanyiwa na makundi ya watu.

Zaidi ya nchi 30 za Afrika, ikiwemo Uganda, tayari zimepiga marufuku mahusiano ya jinsia moja. Sheria mpya inaonekana ni ya kwanza kuwafanya wale watakao jitambulisha kama wasagaji, mashoga, jinsia mbili, na waliobadilisha jinsia (LGBTQ), kuwa wanavunjasheria kwa mujibu wa kundi la Human Rights Watch.

Wafuasi wa sheria mpya wanasema sheria hiyo inahitajika kuwaadhibu wanaojishughulisha na harakati za LGBTQ, ambazo wanasema zinatishia maadili ya kitamaduni ya kikonsevative na kidini katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Kwa kuongezea na mapenzi ya jinsia moja, sheria inapiga marufuku kuhamasisha na kuunga mkono ushoga ikiwemo njama za kujihusisha na ushoga.

Atakaye kiuka sheria hiyo ataadhibiwa vikali ikiwa ni pamoja na hukumu ya kifo kwa kile walicho kiita ushoga uliokithiri, na kifungo cha maisha jela kwa wale watakao patikana na tuhuma za kufanya ngono za kishoga.

Kundi jingine ni wale watakaodaiwa kuhusika na ushoga uliokithiri na kufanya ngono na watoto walio na umri wa chini ya miaka 18 au wakati mhusika anayefanya kitendo hicho ana HIV miongoni mwa sababu nyingine, kwa mujibu wa sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live