Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malema aitaka ICC imtie mbaroni Netanyahu kwa mauaji ya Gaza

Nitasambaza Silaha Kwa Urusi   Asema Julius Malema Wa Afrika Kusini Malema aitaka ICC imtie mbaroni Netanyahu kwa mauaji ya Gaza

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Afrika Kusini ametoa mwito kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kumtia mbaroni Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na mashambulizi ya kinyama yanayoandelea kufanywa na utawala huo pandikizi katika Ukanda wa Gaza.

Julius Malema, kinara wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) alitoa mwito huo jana Alkhamisi wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Wanamajimui wa Afrika katika Chuo Kikuu cha Lukenya, kaunti ya Makueni mashariki mwa Kenya.

Malema ameeleza bayana kuwa, kuna haja kwa mahakama ya ICC yenye makao yake makuu mjini The Hague nchini Uholanzi kuchukua hatua ya kuiwajibisha Israel kwa jinai inazofanya dhidi ya Wapalestina huko Gaza.

Kadhalika kiongozi huyo mashuhuri wa upinzani nchini Afrika Kusini sanjari na kukosoa ziara ya majuzi ya Mfalme Charles wa Tatu wa Uingereza mjini Nairobi, amesisitiza kuwa London inapasa kuwafidia Wakenya ambao ama waliuawa, kujeruhiwa au kupoteza mali zao katika enzi za ukoloni. Ukatili wa Wazayuni katika Ukanda wa Gaza

Jumanne iliyopita, Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Naledi Pandor wakati wa hotuba yake kwenye Bunge la nchi hiyo, aliitaka ICC kuuwajibisha utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na vitendo vyake vya ukiukaji wa sheria za kimataifa wakati utawala huo ukiendelea kufanya jinai dhidi ya binadamu katika Ukanda wa Gaza.

Matamshi hayo yalitolewa siku moja baada ya Afrika Kusini kuwaita nyumbani wanadiplomasia wake wote waliokuwa Israel kulalamikia jinai zinazoendelea kufanywa na Wazayuni Gaza.

Afrika Kusini ambayo ni muhanga wa mfumo wa ubaguzi wa rangi wa apartheid, daima imekuwa ikiwatetea na kuwanga mkono wananchi madhulumu wa Palestina.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live