Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malawi yasitisha safari zote za serikali za nje ya nchi

Malawi Yasitisha Safari Zote Za Serikali Za Nje Ya Nchi Malawi yasitisha safari zote za serikali za nje ya nchi

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amesitisha safari zote za kimataifa zinazomhusisha yeye na maafisa wote wa serikali.

Pia amewaagiza mawaziri wote walioko nje ya nchi kwa sasa kurejea nyumbani.

Akihutubia taifa kupitia televisheni Jumatano usiku, pia alitangaza vikwazo vya usafiri wa ndani na kupunguza kwa nusu ya mgao wa mafuta kwa mawaziri na maafisa wakuu wa serikali.

Hatua hizo zitadumishwa hadi mwisho wa mwaka wa fedha mnamo Machi 2024.

Baadhi ya hatua kama hizo za kubana matumizi pia zilitangazwa wakati wa janga la Covid lakini zilikuwa na athari ndogo kwani hazikutekelezwa kikamilifu.

Rais alimtaka waziri wa fedha kuweka masharti ya nyongeza ya mishahara kwa watumishi wote wa umma katika mapitio yajayo ya bajeti.

Chanzo: Bbc