Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79

Malawiiiiiiiiiiiiiiiiii.png Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Malawi imeondoa vikwazo vya viza kwa wasafiri kutoka mataifa 79 katika juhudi za kukuza utalii na biashara nchini humo.

Waziri wa usalama wa ndani, Ken Zikhałe, katika notisi kwenye gazeti la serikali siku ya Jumatano, alifanyia marekebisho kanuni za uhamiaji, na kuondoa vizuizi vya visa kwa raia kutoka Uingereza, China, Urusi, Ujerumani, Australia, Canada, Ubelgiji, Ghana, Gambia, Sierra Leone, Ufaransa na nchi nyengine.

Raia kutoka nchi za Jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika (Sadc) na soko la pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (Comesa) pia wameondolewa vikwazo hivyo vya viza.

Hatua hii ya serikali haijumuishi nchi zinazowataka raia wa Malawi kuwa viza wakati wakizuru mataifa hayo.

Ubalozi wa Uingereza nchini Malawi uliwataka raia wake kuchukua fursa hiyo ya serikali kutembelea vivutio vingi vya utalii katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

Malawi inaungana na Kenya na Rwanda kufungua nchi zao kwa wasafiri kutoka barani Afrika bila vikwazo vya visa.

Nchi hizo mbili za Afrika Mashariki zimetangaza kuingia bila visa kwa wageni kutoka bara Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live