Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malawi yaomba msaada kutafuta ndege iliyopotea na Makamu wa Rais

Lazarus Chakwera 1 860x593 Malawi yaomba msaada kutafuta ndege iliyopotea na Makamu wa Rais

Tue, 11 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Lazarus Chakwera amesema serikali yake imewasiliana na nchi majirani na washirika wa maendeleo kwa ajili ya kusaidia kuitafuta ndege ya kijeshi iliyokuwa imembeba Makamu wa Rais Saulos Chilima na watu wengine 9 iliyopotea Juni 10.

Katika hotuba kwa taifa kuhusu kupotea kwa ndege hiyo Rais Chakwera amesema serikali yake imewasiliana na serikali za Marekani, Israel, Norway na Uingereza kwa ajili ya uwezekano wa msaada.

Kwa mujibu wa Rais huyo washirika wa maendeleo wameahidi kutoa msaada wa aina mbalimbali ukiwemo matumizi ya teknolojia yatayoongeza uwezo wa kuipata ndege mapema.

"Najua kuwa hii ni hali ya kusikitisha. Najua kuwa sote tunaogopa na tunahofu. Nami nina wasiwasi. Lakini nataka kuwahakikishia kuwa tutatumia kila aina ya uwezo tulionao ili kuipata ndege, na ninasalia na matumaini yote kuwa tutawapata watu wakiwa hai," amesema Chakwera.

Ndege hiyo ikiwa na Makamu wa Rais iliondoka mji mkuu wa Malawi, Lilongwe ikielekea mji wa Kaskazini wa Mzuzu kwenye maziko ya Waziri wa zamani wa Sheria na Mwanasheria Mkuu, Ralph Kasambara aliyefariki ghafla Juni 7.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live