Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malawi yalaumiwa kwa kutopiga kura usitishwaji vita Israel- Gaza

IDF Yasema Imefanya Mashambulizi 250 Ya Anga Gaza Malawi yalaumiwa kwa kutopiga kura usitishwaji vita Israel- Gaza

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashirika ya kutetea haki za kiraia nchini Malawi yamelaani serikali yao kwa kuamua kujizuia kupiga kura ya kutaka kusitishwa vita vya mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina huko Gaza.

Azimio hilo la Jumanne la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lililenga pia kuhakikisha ulinzi wa raia, haswa wanawake na watoto, na kuzingatia majukumu ya kisheria na kibinadamu huko Gaza.

Mashirika ya kiraia yakiwemo Muungano wa Watetezi wa Haki za Kibinadamu (HRDC) na kikundi kingine cha Vijana na Jamii (YAS) yameelezea kujizuia Maliwa kupiga kura kuwa ni hatua 'ya kutowajibika, unafiki, na pia aibu."

Mkurugenzi Mtendaji wa Vijana na Jamii Charles Kajoloweka amesema hatua hiyo ya Malawi ni kupuuza wajibu wake wa kimaadili kimataifa kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa.

Michael Kaiyatsa, ambaye anaongoza Kituo cha Haki za Kibinadamu na Marekebisho ameutaja uamuzi wa serikali ya Malawi kuwa wa kushtua, akisema unafichua unafiki wa serikali.

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zilipitisha azimio la kutaka kusitishwa mara moja mapigano huko Gaza, kuachiliwa mara moja na bila masharti mateka wote, na kuhakikisha ufikiaji wa misaada ya kibinadamu kwenye eneo lililozingirwa.

Nchi 153 ziliunga mkono azimio hilo, 10 zillipinga, huku 23 zikijizuia kupiga kura zikiwemo nchi tano za Afrika ambazo ni Malawi, Cabo Verde, Togo, Cameroon, na Sudan Kusini. Rais Lazarus Chakwera

John Kabaghe, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi, amesema haoni kosa lolote kwa Malawi kutopiga kura.

Hata hivyo, mwanaharakati wa haki za binadamu Malawi, Gift Trapence, ambaye pia ni mwenyekiti wa Muungano wa Watetezi wa Haki za Kibinadamu, amesema hatua hiyo ya serikali ya Malawi hailingani na nchi ambayo ina kiti katika Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa.

Tangu kuingia madarakani mwaka 2020, sera ya kigeni ya serikali ya Rais Lazarus Chakwera imekuwa ikipinga Palestina, ikiwa ni pamoja na kuzuia kuwajibishwa utawala dhalimu wa Israel.

Chakwera, mhubiri wa zamani wa injili, hata ametangaza nia yake ya kufungua ubalozi huko Al Quds (Jerusalem), mpango ambao bado haujatekelezwa. Aidha Malawi imetangaza kutuma wafanyakazi kwenda kutumika katika mashamba yaliyo katika ardhi ambazo zimetekwa na utawala ghasibu wa Israel, hatua ambayo imelaaniwa vikali kote Malawi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live