Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malawi yaharibu chanjo 19,000 za Covid 19,zadaiwa kupitisha muda wa matumizi

Df53cac9d8a3e276 Malawi yaharibu chanjo 19,000 za Covid 19,zadaiwa kupitisha muda wa matumizi

Thu, 20 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Kufikia sasa zaidi ya Raia 330,000 nchini Malawi wamepokea chanjo ya AstraZeneca, hii ni kwa mujibu wa wizara ya afya nchini humo.

Hata hivyo, imeripotiwa kwamba zaidi ya dozi 19,000 za chanjo hiyo zimeharibiwa na mamlaka ya afya kwa madai kwamba zimepitisha muda wa matumizi kwa hivyo ni hatari kwa afya ya wananchi.

Kulingana na Shirika la Afya Duniani, nchi hiyo sasa ni ya kwanza Barani Afrika kuharibu hadharani chanjo zilizopitisha muda wa matumizi.

Aidha, serikali ya Malawi imesema kwamba hatua hiyo inanuia kuwapa raia wake imani ya kuchanjwa dhidi ya ugonjwa huo wakati unaostahili.

Imeripotiwa kwamba idadi chache ya raia wa nchi hiyo wamepokea chanjo hiyo wengi wakihofia zaidi kuhusu habari potofu iliyosambazwa kuhusiana na matumizi ya chanjo hiyo.

Kwa sasa, serikali ya Malawi inaamini kwamba asilimia kubwa ya wananchi itapokea chanjo hiyo shehena nyingine itakapotua nchini kutoka Covax.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke