Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malawi yafunga shule kwasababu ya kimbunga Freddy

Malawi Yafunga Shule Kwasababu Ya Kimbunga Freddy Malawi yafunga shule kwasababu ya kimbunga Freddy

Mon, 13 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Mamlaka nchini Malawi imefunga shule katika wilaya 10 kutokana na wasiwasi wa usalama baada ya Kimbunga Freddy kusababisha uharibifu katika nchi jirani ya Msumbiji.

Mvua kubwa iliyonyesha kusini mwa Malawi imesomba barabara na kutatiza uzalishaji wa umeme, huku mvua zaidi ikitarajiwa kunyesha katika siku chache zijazo.

Masomo yamesimamishwa kwa Jumatatu na Jumanne katika taasisi zote za masomo katika eneo hilo.

Walimu na wanafunzi wamehimizwa kutumia majukwaa yanayopatikana mtandaoni na masomo ya redio, wizara ya elimu ilisema katika taarifa.

"Masomo ya darasani yanapoanza tena walimu wanahimizwa kutoa masomo ya kurekebisha ili kurejesha muda uliopotea," iliongeza.

Nchi jirani ya Msumbiji imepokea mvua ya zaidi ya mwaka mmoja katika wiki nne zilizopita huku Kimbunga Freddy kikitua Jumapili kwa mara ya pili katika mwezi mmoja.

Idadi ya vifo nchini Msumbiji ni takribani watu 28 tangu dhoruba hiyo ianguke kwa mara ya kwanza.

Chanzo: Bbc