Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malawi wamlilia Hayati Magufuli

Jpmm Malawi wamlilia Hayati Magufuli

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: ippmedia.com

Wananchi hao wanasema kiongozi huyo amelifanyia maendeleo makubwa Taifa la Tanzania katika kipindfi kifupi na kwamba baadhi ya maendeleo hayo yamewanufaisha hata wao ikiwemo barabara ya Mpemba-Isongole.

Mmoja wa wananchi hao, Meshack Mkondya alisema kifo cha Dk. Magufuli kiliwashtua kutokana na kwamba hawakuwahi kusikia kwamba alikuwa anaumwa.

Amesema kiongozi huyo amejenga daraja linalounganisha nchi hizo mbili ambalo linawasaidia kusafiri bila shida kutoka nchini kwao kwenda katika miji ya Tunduma, Isongole na Mpemba kununua bidhaa mbalimbali.

“Hili daraja litatufanya tumkumbuke sana huyu kiongozi, tumekuwa tukisafirisha mazao yetu kuja kuuza kwenye soko la Isongole kwa kupitia kwenye hili daraja, lakini hata barabara hii inatusaidia sana,” amesema Mkondya.

Naye James Pili ambaye alikuwa anazungumza zaidi lugha ya Kichewa, amesema Rais Magufuli alikuwa mchapakazi ambaye anastahili kuigwa na viongozi wengine wa mataifa ya Afrika kwa maelezo kuwa ndani ya muda mfupi wa uongozi wake amelibadilisha taifa la Tanzania.

Chanzo: ippmedia.com