Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malawi: Idadi ya vifo kutokana na kipindupindu yavuka 1,000

Malawi: Idadi Ya Vifo Kutokana Na Kipindupindu Yavuka 1,000 Malawi: Idadi ya vifo kutokana na kipindupindu yavuka 1,000

Wed, 25 Jan 2023 Chanzo: Voa

Mlipuko wa kipindupindu nchini Malawi umeua zaidi ya watu 1,000, wizara ya afya imesema Jumanne wakati ambapo nchi hiyo inakabiliwa na uhaba wa chanjo.

Taifa hilo la Kusini mwa Afrika limekuwa likikabiliana na mlipuko wake mbaya wa kipundupindu ambao haujawahi kutokea, huku zaidi ya watu 30,600 wakiambukizwa ugonjwa huo tangu visa vya kwanza viliporipotiwa mwaka jana.

Mwezi Novemba, Malawi ilipokea dozi milioni 3 za chanjo ya kipindupindu inayotolewa kwa njia ya mdomo kutoka Umoja wa mataifa kuanzisha kampeni lakini idadi ya maambukizi inazidi kuongezeka.

“Tumetumia chanjo zote tulizokuwa nazo,” msemaji wa wizara ya afya Adrian Chikumbe ameiambia AFP.

Idadi ya vifo ilifikia 1,002 Jumanne, na kuvuka idadi ya hapo awali ya mlipuko huo mkubwa, ambao uliua watu 968 kati ya 2001 na 2002, kulingana na shirika la afya duniani (WHO).

Chanzo: Voa