Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makundi ya upinzani yashutumu wanajeshi wa serikali mauaji Ethiopia

Makundi Ya Upinzani Yashutumu Wanajeshi Wa Serikali Mauaji Ethiopia Makundi ya upinzani yashutumu wanajeshi wa serikali mauaji Ethiopia

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Wakazi na makundi ya upinzani wameshutumu wanajeshi wa serikali katika eneo kubwa zaidi la Oromia nchini Ethiopia kwa kuwaua raia huku jeshi likiendelea kupambana na wanamgambo katika eneo jingine la Amhara nchini humo.

Kwa mujibu wa wanafamilia wa waathiriwa kutoka eneo la Oromia la Shoa Magharibi waliozungumza na idhaa ya BBC ya Afaan Oromoo, takriban raia kumi wakiwemo wanne wa familia moja waliuawa na vikosi vya serikali.

Juhudi za BBC kupata jibu kutoka kwa serikali ya eneo hazijafanikiwa.

Kundi lenye silaha la Oromo Liberation Army (OLA) linaendesha shughuli zake nyingi katika eneo hilo lakini kulingana na Ararsa Yadesa, watu wanne wa familia yake pamoja na wafanyakazi wawili wa shambani katika kijiji chake waliuawa katika tukio moja, hakukuwa na mapigano kati ya OLA na vikosi vya serikali kabla ya shambulio hilo.

Katika tukio jingine, mwanafunzi wa chuo kikuu alisema yeye na vijana wengine watatu walichukuliwa na vyombo vya ulinzi na usalama kutoka kijijini kwao na yeye pekee ndiye aliyefanikiwa kunusurika baada ya vyombo vya usalama kuwafyatulia risasi.

Vyama viwili vya upinzani, Oromo Liberation Front (OLF) na Oromo Federalist Congress (OFC) viliishutumu serikali kwa mauaji, kukamata watu wengi na ukiukaji wa haki za binadamu huko West Shoa. Vikundi hivyo vimesema idadi ya vifo kuwa 11.

Haya yanajiri huku serikali ikikabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa wanamgambo wenye silaha katika eneo la pili kwa ukubwa la Amhara nchini humo. Wakati hali ya kawaida ikiendelea katika miji mikubwa ya Amhara baada ya mapigano makali ya mijini wiki iliyopita, wanamgambo bado wanadai kudhibiti miji midogo na vijiji.

Chanzo: Bbc